Aunty Ezekiel: Nikiachana na Iyobo itabaki siri

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel, amesema maisha ya mahusiano yake na mzazi mwenzake, Mose Iyobo, yapo kwenye mikono salama ingawa wapo wachache wanaoamini wawili hao hawana maelewano.

Aunty Ezekiel ameliambia DIMBA Jumatano kuwa hata ikitokea ameachana na Iyobo itabaki kuwa siri yao.

“Wapo wengi wanaamini sisi hatuwezi kudumu, lakini nataka niwathibitishie kuwa mapenzi yetu yapo salama sana, tumejiwekea mikakati yetu ili kuhakikisha tunaishi kama tunavyotaka na si kama wengine wanavyotaka na hata ikitokea tukiachana naamini itabaki siri ya sisi wawili,” alisema Aunty.

Aunty alisema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuongeza mtoto kwa kuwa ni wakati sahihi kwake na mwenzake kufanya hivyo, kama ambayo walikuwa wamepanga toka awali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.