NYOTA YAKO WIKI HII

Dimba - - Sultan - Mtabiri Mashuhuri Afrika Mashariki Ramadhani Yahya, pia anatatua matatizo ya kidunia, anapatikana Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam. Simu namba 0652 545462

MBUZI (CAPRICON) Desemba 22-Januari 20

Unatarajia kuanza maisha mapya yatakayokuja na baraka zake, kipato kitaongezeka na pia matarajio mengi sasa yatatimia.

NDOO JANUARI Jan 20-Feb 18

Usiamini ahadi utakazopewa siku ya leo na kesho, hazitatimia, unayemwamini sana atakuangusha wiki hii, kama ulikuwa ukitafuta kitu umefikia wakati wa kukamilisha mipango.

SAMAKI (PISCES) 18-Machi 20

Bahati kwako ipo vizuri ila bado utasumbuliwa na maradhi usiyojua asili yake, hizi ni dalili za nyota yako kukuepusha kuingia katika matatizo mazito.

PUNDA Machi 20-Aprili 20

Jambo lilikushinda siku nyingi kulitatua, litaelekea kufikia (SAGITARIUS) mwisho katikati ya wiki hii, ila kuna habari kubwa Novemba itakayokushtua, jaribu kujenga ujasiri na usiwe na tabia 23-Desemba 21 ya kuongea siri zako na kila mtu.

NG'OMBE (TAURUS) Aprili 20- Mei 21

Tatizo lako ni kusema kila jambo lako kwa kila mtu, hapa ndipo palipoingia uadui ambao sasa utakugharimu.

MAPACHA (GEMINE) (Gemine) Mei 21-Juni 21

Itakuwa ngumu, lakini ukiweza kumuepuka mpenzi wako huyu mrefu kiasi utapata ahueni, nyota zenu haziendi sawa na ndiyo maana kila unalofanya halikamiliki.

KAA (CANCER) Juni 21-Julai 23.

Unaona mafanikio yanakuja polepole, lakini una nafasi ya kuyakaribisha kwa kasi zaidi, tafuta mbinu za kinajimu, yaonyesha huelewi aina ya shughuli zinazoweza kukuongezea kipato zaidi ya sasa.

SIMBA (LEO) JULAI 23-AGOSTI 23

Waliotaka kukwamisha mipango yako, wameshindwa fanya sasa lile ulilokusudia kuna bahati inayokuja mbele yako, jaribu kutafuta ushauri wa kinyota.

MASHUKE (VIRGO) Agosti 23-Septemba 23

Vikwazo sasa vimekwisha na mafanikio yanakuja kwa kasi ila utasikia habari itakayokukatisha tamaa.

MIZANI (LIBRA) AgostiSeptemba 23

Penzi unalotaka kuingia, lina faida kubwa kwako utasahau kero za miaka mingi, lakini utasumbuliwa na wivu kati yenu, mwenzako hapendi kuzungumza sana, mipango ya fedha itasuasua.

NGE (SCROPION) Oktoba 23-Novemba 22

Kipindi hiki ni kizuri sana kwako, utaingia katika penzi zito, lakini siku chache utajisikia kuugua, usihofu tafuna mti wa mkangaa changanya na mkaa wakati wa asubuhi utaona afya yako ikitengemaa.

MSHALE (SAGITARIUS) Novemba 23-Desemba 22

Tembelea ndugu za jamaa au toa sadaka kwa watu wenye mahitaji maalumu, nyota yako inahitaji kutoa faraja kabla mwaka huu haujakatika.

Mtabiri Mashuhuri Afrika Mashariki Ramadhani Yahya, pia anatatua matatizo ya kidunia, anapatikana Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam. Simu namba 0652 545462

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.