MAJIBU YA WIKI ILIYOPITA

Dimba - - Sultan -

Wiki iliyopita kulikuwa na mada inayozungumzia, je, ni nani ataibuka bingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Michuano hiyo ya kuadhimisha kilele cha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, hufanyika kila mwaka visiwani humo ikishirikisha timu mbalimbali za Zanzibar na Tanzania Bara.

Kwa timu za Bara zinazoshiriki kila mwaka ni Simba, Yanga na Azam ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo wakitwaa mara mbili kwa miaka miwili iliyopita.

Wachangiaji wengi walituma maoni yao juu ya suala hilo huku asilimia kubwa wakiamini Azam anatetea taji lake na kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo wakiipa nafasi kubwa ukilinganisha na wapinzani wake.

Mimi naitwa Alexa Lyakurwa wa Posta Mpya, mtazamo wangu Azam watachukua kombe la Mapinduzi, kwa sababu wana kikosi kizuri na kocha bora ambaye aliwahi kubeba makombe yote akiwa na Yanga.

Naitwa Michael Moses wa Iringa Mjini, Kombe la Mapinduzi bila shaka Azam wanahusika, Simba na Yanga hawana jeuri hiyo japo mie ni shabiki sana wa Yanga.

Naitwa Evod Magidanga wa Tanga, kwangu mie naona bingwa wa Kombe la Mapinduzi ni Azam kwa sababu hizo, kwanza aina ya wachezaji waliokwenda nao kwenye mashindano ni tofauti na timu nyingine hasa wapinzani wake wakuu, Simba na Yanga, pili Azam anahitaji kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Naitwa Izraely Kitomary, kulingana na ubora wa kikosi cha Simba, nina kila sababu ya kusema wanaweza kutwaa ubingwa huo.

Naitwa Zungi Zee wa Tabata, mimi naona Kombe la Mapinduzi bingwa mtetezi (Azam) ndiye atalitwaa tena japo mimi ni Yanga damu.

Naitwa Joel Mwalonde wa Mkamba, mimi naamini Simba itatwaa kombe hilo kwani wana kikosi kipana na kina uwezo mzuri.

Naitwa Joseph Odomu wa Kibamba Hospital, bingwa wa mwaka huu Mapinduzi ni Simba kutokana na ubora wa kikosi chake.

Naitwa Mohamed Kayombo, mimi naamini timu ambayo imepeleka kikosi kamili na kujipanga kwa ajili ya mashindano ndiyo itakayoweza kutwaa taji hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.