Maumivu-20

ILIPOISHIA... “Uko wapi?” Alikuwa ni Emma akiongea, baada ya kumpigia simu Vanessa. “Kariakoo!” “Wapi sasa?” “Dukani!” “Ok! Nilitaka kukupa mwaliko mpenzi wangu.” “Mwaliko? Wa nini?” “Nataka kutoka na wewe kwa ajili ya chakula cha jioni!” “Mwenyewe au na

Dimba - - Sultan - ITAENDELEA... Je, nini kitatokea? Usikose wiki ijayo. Karibu kwa maoni yako 0718-400146.

YALIKUWA maajabu makubwa sana kwa Emma, mwanamume yule mkorofi, mwenye maneno mengi, vipigo na lawama kila siku, leo amekuwa wa outing, zawadi, maneno ya mapenzi na kila kitu kizuri kwa ajili ya kuboresha mapenzi. Hakika ni jambo la heri sana!

Vanessa alishangazwa sana na Emma wa siku hizi, amebadilika na anajua kuheshimu hisia zake. Ilikuwa maajabu sana! Maajabu yaliyomuacha njiapanda. Maana alikuwa na wawili; Bruno na Emma.

“Nitajua cha kufanya,” akajisemea mwenyewe akilini mwake.

Lakini alijiandaa kwa ajili ya chakula cha jioni na Emma, mpenzi wake.

***

Kijani kibichi cha Tobis Hotel, kilionekana vizuri sana. Taa za rangi zilizozunguka mandhari ile, zilizidi kuongeza mwonekano wa kuvutia eneo lile. Maji yaliyokuwa yakitiririka kwenda kwenye mabwawa ya kuogelea pia yalizidisha utulivu wa Tobis Hotel.

Emma anashuka kwenye gari, macho yake yakiangalia vizuri Hoteli hiyo nzuri iliyopo Sinza, Afrika Sana, jijini Dar es Salaam. Vanessa naye anashuka, wanakutana na kushikana mikono.

Kushoto kwao kulikuwa na meza, kulia vivyo hivyo! Vanessa anamvutia kulia, lakini Emma anamvutia upande wa kushoto. Wanavutana. Mwisho Emma akaibuka mshindi, maana alikuwa akimvuta kwa kutumia nguvu zaidi.

“Umeshinda,” Vanessa akasema akimfuata Emma kwa nyuma.

Wakaketi kwenye viti vizuri, vikubwa, vilivyotengenezwa kwa mkeka halisi. Muda mfupi tu baadaye akatokea mhudumu na kuwasikiliza. Wakaweka oda ya chakula na kuletewa vinywaji, wakaendelea kunywa.

“Hivi unafahamu sababu hasa ya kukutoa usiku huu baby?” Emma akamuuliza Vanessa.

Vanessa akashtuka sana! Swali tata! Kwake lilikuwa na maana mbili, kwamba yawezekana anamuuliza hivyo, lakini jibu ni kwamba alimtoa ili amuulize kuhusu uhusiano wake na Bruno! Hakujiamini hata kidogo katika hilo.

“Hapana sweetie, sijui!”

“Kwa ajili ya kitu kimoja tu, kuendelea kuboresha penzi letu. Nafahamu kwamba nimekuwa nikikutesa kwa muda mrefu sasa, ni wazi kwamba huenda kichwani mwako unawaza kuachana na mimi, lakini nataka kukuhakikishia kwamba sitakuumiza tena, sitakutesa na sitakufanyia lolote baya kwa mara nyingine tena.

“Ni kweli kwamba sikuwa mwanamume mwema kwako, lakini nataka kukuhakikishia kwamba, nimeamua kubadilika moja kwa moja, sitaki tena kugombana na wewe. Nimeshatambua makosa yangu na najua kwamba natakiwa kukufanya uwe na furaha wakati wote. Nakupenda sana mpenzi wangu,” akasema Emma kwa sauti iliyojaa utulivu.

Vanessa alikaa kimya akimsikiliza, maneno yake yalimwingia sana. Kimsingi Emma hakuwa na haja ya kuzungumza sana, kwani matendo yake yalitosha kabisa kuonesha anamaanisha nini. Emma alibadilika kwa kila kitu, alifaa kabisa kuitwa mume! Tatizo ni Bruno! “Nimekuelewa mpenzi wangu, nimefurahi kusikia ukitamka kwa kinywa chako kwamba ulikuwa unanikosea, lakini pia nimefurahishwa na jinsi ulivyoahidi kubadilika. Kuna kitu kimoja ambacho hujakijua... tayari umeshabadilika kwa muda mrefu sasa, naona mabadiliko yako na nataka kusema kwamba yananifurahisha sana mpenzi wangu. Nashukuru kwa kila kitu mpenzi.” “Ahsante sana!” Wakaendelea kunywa huku wakisubiri chakula, Emma hakujua kabisa kwamba Bruno hakuwa ‘Anko’ kama alivyotambulishwa, bali alikuwa mpenzi. Kilichokuwa mbele yake kwa wakati huo ilikuwa ni kuongeza mapenzi ya dhati kwa Vanessa ili azidi kumpenda! *** MIEZI MITATU BAADAYE

Kichwa chake kilivurugika kabisa, siku zilivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kugundua mambo mapya. Leo amegundua jipya kabisa. Kwamba kumbe hampendi Vanessa! Mapenzi yake na Emma yanamchanganya sana. Wanaelewana, kwahiyo nafasi yake kwa Vanessa inazidi kupungua taratibu.

Kama hiyo haitoshi, hata yeye ndani ya moyo wake, alionekana kuanza kumkumbuka mke wake mpenzi aliyemuacha Mwanza. Akawaza familia yake.

“Natakiwa kufanya kitu,” akawaza Bruno kichwani mwake.

Hakuwa na jambo lingine zaidi ya kufikiria kurudi nyumbani kwake Mwanza, tatizo lilikuwa deni analodaiwa na kampuni aliyokuwa akifanyia kazi.

“Mungu wangu na pesa za watu?” Akawaza Bruno akiwa hana jibu.

“Yeah! Nimeshajua cha kufanya,” akajijibu ghafla. *** Siku nzima Bruno alikuwa na mawazo, hakuweza kuwahudumia wateja wake vizuri, akili yake yote ilikuwa ni juu ya mkewe Mwanza. Wazo alilolipata usiku wa kuamkia siku hiyo, aliamua alitumie. Akachukua simu yake na kumpigia Vanessa. Akamwomba akutane naye mahali mchana huo.

“Kuna nini?” Vanessa akauliza.

“Ni muhimu sana, naomba tukutane tafadhali.” “Hapo dukani vipi?” “Nitafunga.” “Hapana, napitia hapo sasa hivi.” “Sawa!” Nusu saa baadaye Vanessa alikuwa ameshafika dukani, akamkuta Bruno akiwa na mawazo sana. Akaishangaa sana hali hiyo.

“Vipi mwenzetu, mbona hivyo?” “Mawazo Vanessa.” “Juu ya nini?” “Wanangu. Nahitaji kwenda kuwasalimia, lakini nashindwa kabisa. Kuna kitu nahitaji msaada wako.” “Sema ni nini?” “Ili niweze kwenda Mwanza, lakini nipeleke na zile fedha za watu, tafadhali naomba unisaidie!”

“Unataka shilingi ngapi Bruno.”

“Nadaiwa milioni nne, lakini naamini hata nikiwapelekea tatu na kuwaahidi iliyobaki watanielewa.”

“Kwahiyo unataka milioni tatu?” “Ndiyo!” “Usijali nitakupa milioni kumi, ulipe deni la watu, lakini pia uweze kuwa na balance ya kutatua matatizo madogo madogo huko nyumbani!” Vanessa akasema kwa sauti tulivu sana.

Bruno akachanganyikiwa.

Akachanua tabasamu!

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.