Wachana nyavu wanaotolewa macho na Barcelona hawa hapa

Dimba - - Sport Pesa -

WAKATI timu kadhaa barani Ulaya zikiwa ‘bize’ kutumia vema dirisha dogo la usajili kuvuta majembe mapya majira haya ya baridi, Barcelona pia wana mikakati mizito ya kusaka mashine za mabao. Mastraika wanaosakwa ni mbadala wa baadaye wa kina Luis Suarez ambaye umri unampiga mkono, miaka 32, lakini pia shujaa wa viunga hivyo, Lionel Messi akiwa katika kapu hilo. Nyota wanaotajwa kuvutwa kikosini hapo ambapo zoezi hilo litafanyika majira ya kiangazi, ni Krzysztof Piatek (Genoa), Nicolas Pepe (Lille), Maxi Gomez (Celta Vigo), Luka Jovic (Eintracht Frankfurt) na Timo Werner (RB Leipzig). Miongoni mwa wakali hao watakaofanikiwa kumwaga wino viunga hivyo wataungana na Paco Alcacer anayekipiga kwa mkopo Borussia Dortmund pamoja na Munir El Haddadi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.