Salamba: Wanasimba jiandaeni kupokea kombe

Dimba - - Mbele -

NA SAADA SALIM, ZANZIBAR STRAIKA wa Simba, Adam Salamba, amewaambia mashabiki wa kikosi hicho wajiandae kupokea ubingwa wa michuano ya Mapinduzi ambayo inafikia tamati leo.

Simba wametinga fainali na leo watacheza na mabingwa watetezi Azam FC, mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utakaochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba.

Wekundu hao wa Msimbazi wameingia fainali baada ya kuwafunga Malindi kwa mikwaju ya penalti 3-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan, Unguja.

Akizungumza na DIMBA, Salamba alisema wao kama wachezaji wamejiandaa vizuri kuwapa furaha mashabiki hivyo wamiminike kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti.

“Najua ni mchezo mgumu kwani tunakutana na Azam ambao licha ya kwamba ni mabingwa watetezi, wanacho kikosi kizuri lakini kwa upande wetu tumekuja kwa kazi moja tu kuhakikisha tunaondoka na ubingwa.

MATUMAINI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.