Simba Queens, Yanga Princess hapatoshi leo

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

SIMBA Queens na Yanga Princess wametambiana kutoana jasho mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Lite utakaochezwa leo Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha wa timu hizo, Khamis Kinonda wa Yanga Princess na Mussa Hassan ‘Mgosi’, wa Simba Queens, kila mmoja alitamba kikosi chake kuibuka na ushindi.

“Mchezo utakuwa mgumu lakini juhudi za wachezaji ndizo zitakazotufanya tushinde ukizingatia pia tumerekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance Girls,” alisema Kinonda wa Yanga Princess.

Kwa upande wa kocha wa Simba Queens, Mgosi, alisema hawawezi kuwadharau Yanga Princess na kusisitiza mchezo utakuwa mgumu kwani popote inapotokea timu hizo zinakutana hata mchangani huwa nyasi huumia.

Naye nahodha wa Simba Queens, Mwanahamisi Omary, alisema wamepeana majukumu ya kufanya watakapokuwa uwanjani hivyo mashabiki wao wategemee makubwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.