Judo A/Mashariki kupigwa Machi 14

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

MASHINDANO ya judo ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika Machi 14-17 mwaka huu, hapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA, Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (Jata), Innocent Malya, alisema maandalizi yanaendelea vyema na wanaamini mashindano hayo yatakuwa na mwitikio mkubwa.

Alisema klabu zote zinatakiwa kujipanga vilivyo kuhakikisha zinajiandaa kiushindani ili kuiwakilisha vyema nchi yetu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.