UWOYA, DOGO JANJA NI MWENDO WA VIJEMBE TU

Dimba - - Kona ya ubuyu -

BAADA ya ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya kusemekana kwamba imevunjika, wawili hao wanaonekana kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii ikiwa bado hawajathibitisha kuachana kwao mahali popote.

Uzito wa mvutano wa Irene Uwoya na Dogo Janja, unakuja baada ya baba mlezi wa Dogo Janja ambaye ni Madee, kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akisikiliza wimbo wa marehemu msanii, Jack Simela, huku akimtaja Dogo Janja kama anamuusia kuhusu mahusiano ya mapenzi.

Uwoya aliandika..kutoka kufanya hip hop mpaka kwenye taarabu, ooh shame….Dogo Janja naye akaandika…Ni bora uonekane huna pesa kuliko kutumia pesa nyingi uonyeshe na wewe unazo.

INASEMAKENA penzi kati ya staa wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel na mzazi mwenzake, Moses Iyobo, huenda limekwisha kwa sasa kutokana na wawili hao kuishi kila mtu kivyake ama la. huku Iyobo akimwondoa mwenzake kwenye orodha ya marafiki zake kwenye mtandao wa kijamii.

Habari hiyo imesambaa katika kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akishindwa kuweka wazi kama ni kweli wamemwagana

MWIGIZAJI Nisha Bebe, amerudi tena kwenye ‘headlines’ ikiwa ni miaka kadhaa imepita toka atangaze kuachana na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wenye umri mdogo, sasa amerudi tena kwenye kundi hilo la kumiliki vibenteni.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Nisha Bebe, amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kwa sasa yupo mapenzini na mtu ambaye asingetamani kumweka wazi na amemzidi umri na kwa upande wa Watanzania ameshamalizana nao.

Aliandika…“Kuna kitu wacha nikiweke sawa, kuna post niliona kama sio jana basi juzi inasambaa kunihusu sijui nina ‘kibenten’ mpya sijui nini na nini. Wapendwa huko mi nimeshavuka tangu 2016, nilishaapa ‘kutokudate’ na mtu niliyemzidi umri pamoja na kipato na Mtanzania mwenzangu kwangu ni mwiko tena.”

MCHEKESHAJI Mc Pilipili amefanya mahojiano na kipindi cha Redio Clouds FM cha Leo Tena na amezungumza kuhusiana na vitu vingi vinavyomhusu mpenzi wake, Phelomena, ikiwemo na kiasi alichokitoa kwa ajili ya mahari.

Mc Pilipili aliandika….Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa”…. “Ni kweli nimeokoka, ndio maana kwenye sherehe ya kuvishana pete hakukuwa na vinywaji vikali, hatuishi pamoja na mpenzi wangu ila huwa anakuja nyumbani kwangu kupika’’…Mshenga aliniambia mahari ni Sh mil 8 na tulifanya mazungumzo kidogo, hivyo hadi sasa nimetoa Sh mil 5 bado Sh mil mbili.”

BAADA ya kumaliza ziara yao katika nchi za Ulaya, msanii wa hip hop, Ben Pol na mpenzi wake, Anerlisa raia wa Kenya, ambapo walikua wakila bata, sasa wameonekana jijini Nairobi ambapo mpenzi wake huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Ben Pol alishindwa kujizuia na kumwandikia ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram… Happy birthday Mylove.. Nakutakia maisha marefu na furaha..May your dream come true Myqueen.

MTANZANIA Mbwana Samatta ambaye ameendelea kuiwakilisha nchi yake vyema katika soka la kulipwa, ni miongoni mwa wachezaji wanaoongoza kwa idadi ya mabao katika klabu yake huko nchini Ubelgiji.

Bosi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, aliamua kutumia nafasi hiyo kumpongeza na kuzidi kumpa moyo kutokana na juhudi zake huku akiandika…Hongera mshindi kwa jitihada zako kama mfungaji bora huko Ubelgiji…kila siku Watanzania tunajivunia wewe.

STAA wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameamua kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kutangaza kuwa ataanza kugawa nguo zake ambazo mashabiki wanazipenda mwaka huu.

Lulu aliandika…Kuna nguo yangu yoyote umewahi kuipenda na kutamani uwe nayo? Okay…2019 nitaanza kusafisha kabati langu.. nani yupo tayari ???????????

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.