Zijue alama muhimu katika uwanja wa mpira

Dimba - - Kona ya ubuyu -

ATIKA uwanja wa soka kuna alama mbalimbali zimechorwa na kwamba kwa mujibu wa sheria zinazouongoza mchezo huo, kila alama ina maana yake.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezo wa mpira wa miguu unaongozwa na sheria 17 pamoja na kanuni ambazo hutungwa na chama cha mpira.

Uwanja ambao ni kwa ajili ya kutumika kuchezea mpira wa miguu sheria za mchezo huo zinautaka kuwa na alama ambazo waamuzi watazitumia kuuongoza au kuchezesha mchezo huo.

Pamoja na kuwepo kwa alama hizo, lakini zimewekwa kwa vipimo maalumu lengo likiwa hilo hilo la kuwaongoza waamuzi kuuchezesha mchezo kwa kutumia sheria pamoja na alama zilizopo uwanjani pindi mchezo unapoendelea.

Kwa mujibu wa sheria, alama zilizopo uwanjani na vipimo vyake ni kwenye mabano ni mzunguko wa katikati wenye mita 10 (Centre Circle), alama ya katikati (Center Mark), eneo la goli lenye mita 6 (Goal Area).

Vile vile kuna alama yakupigia penalti (Penalty Mark), eneo la penalti lenye mita 12 (Penalty Area), eneo la nje ya penalti lenye mita 10 (Penalty Arc), eneo la kupigia kona lenye mita 1 (Corner Arc).

Alama nyingine ni eneo la goli lenye mita 6 (Goal Area) pamoja na nusu mstari wa katikati (Halway Line) huku eneo la kutoka mlingoti mmoja wa goli kwenda mwingine una mita 8 na urefu wa kwenda juu kwenye mtambaa wa panya ni futi 8.

Pia alama nyingine ni ile mistari miwili mirefu (Touch Line) na ile miwili mifupi (Goal Line).

Sambamba na alama hizo, pia kwenye kila kona ya uwanja kumewekwa milingoti iliyofungwa bendera ambazo ni alama ya kuonyesha mahala ambako uwanja unapoishia na kwamba kila mlingoti mmoja una urefu wa futi 5 kwenda juu.

Kulingana na sheria za mchezo huo, milingoti yote ya magoli pamoja na ile ya vibendera ambavyo vipo kwenye kila kona ya uwanja vinatakiwa kuwa na umbo la duara na iliyotengenezwa kwa matirio laini isiyoumiza.

Ikumbukwe kuwa katika milingoti ya magoli si lazima kuwekewa nyavu lakini ili kuepuka magoli yanayoweza kusababisha utata ni muhimu kuweka.

Kama tulivyoeleza katika toleo lililopita ili uwanja uwe na sifa za kutumika katika michezo mbalimbali ya ligi pamoja na mechi za kirafiki za kitaifa au kima- taifa unatakiwa kuwa na urefu usiozidi mita 130 na usiopungua mita 100 wakati upana wake unatakiwa kuwa mita 100 na usipungue mita 50.

Lengo la kuugawanya uwanja katika nusu mbili zinazolingana kwa kuchorwa mstari katikati ya uwanja ni ili kuzitenganisha timu zitakazokuwa zikicheza kwa wakati huo.

Kwa upande wa ile mistari miwili mirefu (Touch Line) na ile miwili mifupi (Goal Line) ipo kwa ajili ya kuonyesha eneo zima la uwanja ikiwa ni pamoja na kuwawezesha waamuzi kuona mpira wa kutoka, mpira uliovuka mstari wa goli, mpira wa kona pamoja na ule wa kipa kupiga (Goal Kick). Uchambuzi huu wa sheria 17 za mpira wa miguu umeandaliwa na mwandishi wa gazeti hili ambaye pia mwamuzi wa mpira daraja la pili taifa. Kwa maswali, maoni na ushauri katika sheria hizi za mpira tuwasiliane kupitia barua pepe [email protected] yahoo.com

Kulingana na sheria za mchezo huo, milingoti yote ya magoli pamoja na ile ya vibendera ambavyo vipo kwenye kila kona ya uwanja vinatakiwa kuwa na umbo la duara na iliyotengenezwa kwa matirio laini isiyoumiza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.