Gongolamboto walilia fidia ujenzi SGR

Mtanzania - - Habari - Na NORA DAMIAN

ZAIDI ya wakazi 200 wa Mtaa wa Gulukakwalala, Kata ya Gongolamboto wanaotakiwa kupisha ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), wameiomba serikali kuangalia upya viwango vya fidia wanavyotakiwa kulipwa kulingana na eneo hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema wanakubali nyumba zao kubomolewa kupisha ujenzi wa reli hiyo lakini hawakubaliana na fidia wanayotaka kulipwa.

Mmoja wa wakazi hao, Monica Madata, alisema licha ya kumiliki nyumba ya vyumba vinne anashangaa katika uthamini uliofanywa anatakiwa kulipwa fidia ya Sh milioni 1.1.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.