Tafiti za mazingira ziwekwe hadharaniMalongo

Mtanzania - - Tangazo - Na MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Joseph Malongo, ameagiza tafiti zinazofanywa za mazingira zitangazwe ili ziweze kueleweka na wananchi, ili Serikali iweze kufanya uamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, baada ya kufungua warsha kwa wadau wa mazingira iliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kujadili namna bora ya kutekeleza mapendekezo kutoka kwenye tafiti, Mhandisi Malongo alisema tafiti zinasaidia kuonesha matatizo ya kimazingira yaliyopo katika maeneo husika na namna ya kuyatatua.

“Warsha hii ni muhimu kuwapitisha wataalamu wetu kutoka vyuo na taasisi mbalimbali ili waweze kuelewa ajenda ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2017-2022, ili watakapokuwa wanaandaa tafiti zao ziendane na mapendekezo yaliyomo katika ajenda,” alisema Malongo.

Alisema nchi ina wataalamu wengi ambao wamefanya tafiti mbalimbali, ambazo kama zingetangazwa na kufanyiwa utekelezaji, mafanikio makubwa yangepatikana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.