Justin Bieber kufuta ‘tattoo’ ya Selena

Mtanzania - - Habari - NEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber, yupo kwenye mipango ya kufuta tattoo ya mpenzi wake wa zamani, Selena Gomez.

Mipango hiyo imeanza mara baada ya mkali huyo kumvisha pete mpenzi wake mpya, Hailey Baldwin, ambaye anatarajia kufunga naye ndoa.

Bieber amesema baada ya kuachana na Selena, aliamua kuichafua tattoo hiyo ili isijulikane kama ni Selena, lakini bado mashabiki wana kumbukumbu.

“Mashabiki wangu bado wana kumbukumbu na picha na Selena ambayo niliichora kwenye mkono wangu, nilijaribu kuifuta kidogo lakini bado inaonekana kwa mbali na mashabiki wameliona hilo, hivyo ni lazima nifute moja kwa moja kwa kuwa sasa nina mtu mwingine ambaye ameziba nafasi hiyo,” alisema Bieber.

Msanii huyo aliongeza kwa kusema kwa sasa hana mpango wa kuwa kwenye uhusiano na msichana mwingine kwa kuwa moyo wake amempa mpenzi wake wa sasa, Hailey.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.