Mfuko wa Jimbo Bumbuli kuchangia miradi mil 46/-

Mtanzania - - Kanda Ya Kaskazini - Na MWANDISHI WETU

KIASI cha Sh milioni 46.07 kimetengwa na Mfuko wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, mkoani Tanga, kuchangia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zote 18 za jimbo hilo.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba, ilieleza kuwa jumla ya miradi 18 itafaidika na msukumo huo wa fedha hizo kutoka katika mfuko wa jimbo hilo.

Pia ilielezwa kuwa fedha hizo zitatolewa hivi karibuni na maandalizi yake yamekamilika.

Pamoja na hali hiyo, miradi iliyotajwa kuwa itanufaika na fedha hizo ni huduma ya maji, ujenzi wa madarasa, zahanati na matengenezo ya barabara.

“Kwa mfano taarifa hiyo imesema kuwa Kata ya Kisiwani itapata jumla ya Sh milioni 4 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa huduma ya maji, wakati ambapo Kata ya Tamota itapatiwa shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Ngwelo.

“Miradi mingine ni mradi wa zahanati katika Kijiji cha Tekwa ambao mfuko umechangia shilingi milioni 1.44, mradi wa zahanati Kwemsambia saruji yenye thamani ya shilingi 675,000, ujenzi wa darasa Shule ya Msingi Kivilu,” ilieleza taarifa hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.