Washindi wanane wakunja milioni kila mmoja

Mtanzania - - Habari Za Michezo - Na GLORY MLAY

WASHINDI wanane kutoka mikoa mbalimbali nchini, wamejishindia fedha Sh milioni moja kila mmoja, kupitia droo ya kila wiki ya promosheni ya bia ya Kilimanjaro.

Mbali na kujishindia fedha taslimu, promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa Mei mwaka huu, imefanikisha ndoto za Watanzania 10 kwenda nchini Urusi kushuhudia mechi za michuano ya Kombe la Dunia na tayari wamerejea nchini.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema jana lengo la promosheni hiyo ni kuwazawadia wateja wao msimu huu wa Kombe la Dunia, ili kujishindia fedha taslimu Sh 1,000,000 na muda wa maongezi wa Sh 2,500.

Kikuli aliwataka wateja wa bia ya Kilimanjaro kuendelea kuchangamkia promosheni hiyo kwa kuwa umebaki muda mfupi kabla haijafikia tamati.

“Tunafurahi kuona promosheni hii ya kuleta shangwe za Kombe la Dunia kwa wateja wetu, imefanikiwa na inaendelea kuleta shangwe katika msimu huu, tutaendelea kuwaletea promosheni mbalimbali za kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono,” alisema Kikuli.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.