Lomodo: Sina mahusiano na Nandy

Mtanzania - - Habari - NA CHRISTOPHER MSEKENA -DAR ES SALAAM

BAADA ya picha za wasanii wa Bongo Fleva, Leberatus Yeronimo ‘Lomodo’ na Faustina Charles Nandy, kusambaa katika mitandao ya kijamii na kuibua gumzo la wawili hao kuwa katika uhusiano wa kimapenzi, Lomodo amefunguka na kusema hakuna mahusiano yoyote kati yake na mwanadada huyo.

Akizungumza na MTANZANIA, Lomodo alisema Nandy ni rafiki yake wa karibu na picha za kimahaba zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, zimevuja kutoka kwenye kazi yao mpya ambayo amemshirikisha mrembo huyo.

“Zile ni picha tu za kazi yangu mpya ambayo nimefanya na Nandy, mapenzi sidhani kama yapo kati yetu, hivyo mashabiki waache kuunganisha matukio, Nandy ni rafiki yangu na ninamheshimu na kuheshimu uhusiano wake na mpenzi wake,” alisema Lomodo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.