Maonyesho ya Sabasaba yaongezwa siku

Mtanzania - - Habari Za Sabasaba -

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), imeongeza siku za Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yaliyotakiwa kumalizika Julai 13, mwaka huu hadi Julai 15.

Kuongezeka kwa siku hizo mbili kunafanya maonyesho hayo yaliyoanza Juni 28, mwaka huu kudumu kwa siku 18.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tantrade, Edwin Rutageruka, alisema sababu ya kuongeza siku imetokana na maombi ya wadau.

“Maombi haya ya wadau, sisi kama Tantrade kupitia naibu waziri wetu tumekubaliana kuongeza siku mbili mbele ili kuwapa nafasi Watanzania na wadau wengine kupata nafasi ya kutembelea japokuwa kiingilio kitabaki vile vile,” alisema Rutageruka.

Alisema pamoja na maonyesho hayo kuongezwa siku, bado yatafungwa Julai 13 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Rutageruka aliwashukuru washiriki wa nje na wa ndani kwani maonyesho yamekuwa mazuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.