Wavumilieni Wachina, Serikali yawaambia Wakenya

Mtanzania - - Habari Za Kimataifa / Matangazo -

SERIKALI imewataka Wakenya kuwavumilia Wachina, ambao wanakabiliwa na tuhuma za ubaguzi katika uendeshaji mradi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge.

Msemaji wa Serikali Eric Kiraithe alisema juzi kuwa Wakenya wakiwamo wale wanaokabiliwa na ukandamizaji wanapaswa ‘washukuru’ kile Wachina wanachofanya.

Shirika la China Road and Bridge linalojenga na kuiendesha reli hiyo, limekuwa likituhumiwa kuwabagua Wakenya, ambao wanatarajia kuchukua usimamizi wa kutoa huduma kipindi cha miaka 10 ijayo. Ubaguzi huo unahusu eneo la ajira, kazi, mishahara, mpangilio wa kukaa, huduma za chakula na huduma za usafi binafsi kwa kutaja chache.

Lakini bila kufafanua zaidi, Kiraithe alida utawala wa Rais Uhuru Kenyatta umeweka ‘mifumo’ ya kutatua operesheni za huduma za treni za abiria na mizigo ya Madaraka Express.

Alipuiuza tuhuma za kutendewa vibaya lakini aliongeza kuwa uchunguzi wa madai hayo unaendelea.

Badaya ya kuchafua taswira ya mradi huo wa mabilioni ya shilingi, msemaji huyo aliwataka wafanyakazi wa Kenya wawafichue watu binafsi wanaotuhumiwa kuwakandamiza

“Tumeweka hatua zote kushughulika na masuala haya, lakini iwapo u Mkenya unatyedai kutendwa vibaya na hujaripotio polisi wala Fida (chama cha wanasheria), basi fanya hivyo,” alisema Kiraithe.

Wakati akikiri kuwa serikali imepokea malalamiko ya ubaguzi, alisema kwamba hatua zimechukuliwa dhidi ya wageni waliokutwa na kosa la kukandamiza wakenya.

Kiraithe pia aliwalaumu watu ambao hakuwataha kuwa ndio wachawi wanaokwamishwa mradi huo kuelekea Dira ya 2030.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.