Alicia Keys wa Kenya apata dili nono

Mtanzania - - Burudani -

MSICHANA aliyewashangaza wengi kwa kipaji chake cha kuimba wimbo wa nyota wa muziki nchini Marekani, Alicia Keys, amepata dili nono la kusajiliwa na kampuni ya muziki ya Pine Creek Records.

Glorious Amani, ambaye amejulikana kwa jina la Alicia Keys, amesajiliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kukuza kipaji chake. Kampuni hiyo ilitangaza habari hiyo kupitia akaunti yake ya facebook.

“Kipaji chake kimewasili nyumbani ambapo kitatunzwa kwa kiwango cha hali ya juu, ungana nasi katika kumkaribisha Glorious katika lebo yetu ya muziki,” waliandika kupitia ukurasa huo wa Facebook.

Msichana huyo, ambaye anasoma darasa la nne, aligonga vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya video yake inayomwonyesha akiimba wimbo wa ‘Girl On Fire’ ambao uliimbwa na Alicia Keys na video hiyo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na hata Alicia mwenye alionesha kuguswa na kipaji cha mtoto huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.