MBAPPE awajibu England

Mtanzania - - Michezo -

STAA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, amewajibu mashabiki wa England ambao walikuwa wanamtumia ujumbe mfupi wa maandishi kuwa, England haiwezi kurudi nyumbani bila ya Kombe la Dunia. Mbappe amedai mashabiki hao walikuwa wanamtumia ujumbe kwamba, mpira umerudi nyumbani, wakimaanisha kwamba huu ni wakati wa England kuandika historia kwenye Kombe la Dunia na si Ufaransa. Mara ya mwisho England kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1966, tangu hapo hadi sasa timu hiyo haijawahi kufanya vizuri. “England waliniambia haiwezekani kurudi nyumbani bila ya ubingwa, sasa ninaamini inawezekana, samahani lakini kwa kuwa England ninaipenda ila kwa wale walionitumia meseji ambazo hazina maana wanastahili majibu haya,” aliandika Mbappe kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo, ujumbe huo unaonekana kumwongezea idadi kubwa ya maadui baada ya mashabiki wengi kuamua kumshambulia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.