Atozwa faini 500,000/-

Mtanzania - - Kanda -

ALIYEKUWA Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Maalumu Mitindo wilayani Misungwi, Kulwa Ng’hwelo (43) ametozwa faini ya Sh 500,000 baada ya kukutwa na makosa ya rushwa, anaripoti Twalad Salum.

Ng’welo alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya ubadhirifu na ufujaji wa fedha kwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 7.1 kutokana na matumizi ya umeme katika shule hiyo inayotoa elimu jumuishi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Erick Marley, alisema mashahidi sita wa upande wa Jamhuri walithibitisha pasipo na shaka juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili mwalimu huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.