Dondoo

Mtanzania - - Michezo -

Man United UONGOZI wa klabu ya Manchester United, upo kwenye mipango ya kutaka kuachana na mshambuliaji wao, Alexis Sanchez, wakati wa kiangazi mwakani. Wamedai wanaweza kufanya hivyo kutokana na kutofurahishwa na kiwango chake. Chicago BEKI wa klabu ya Chicago Fire, Brandon Vincent, ameishangaza dunia baada ya kutangaza kustaafu soka huku akiwa na umri wa miaka 24. Imekuwa ikizoeleka kuwaona wachezaji wakistaafu kuanzia umri wa miaka 34. Real Madrid KWA mujibu wa mtandao wa Sport, wachezaji wa klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, wanapambana kuhakikisha aliyekuwa kocha wao, Zinedine Zidane, anarudi katika nafasi yake baada ya Julen Lopetegui kufukuzwa. West Ham KIUNGO wa klabu ya Tottenham, Victor Wanyama, anaweza kuonekana akiwa na uzi wa klabu ya West Ham wakati wa Januari mwakani kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya kuitaka saini yake ili kuweza kuongeza nguvu. Real Madrid RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, amelitaja jina la kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, kuwa miongoni mwa makocha ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui ambaye amefukuzwa kazi Jumatatu wiki hii. Real Madrid UONGOZI wa klabu ya Real Madrid, umekanusha taarifa za kuwa timu hiyo ipo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya River Plate, Exequiel Palacios, lakini klabu ya Inter Milan ipo kwenye mipango hiyo. Wolves KLABU ya Wolves, imekutana na Napoli kwa ajili ya kujadili juu ya uwezekano wa kutaka kumsajili Mario Rui pamoja na Amadou Diawara. Hata hivyo, Napoli inaonekana kutokuwa na mpango wowote wa kutaka kuwaacha wachezaji hao wakiondoka. Besiktas WAKALA wa mlinda mlango, Loris Karius, ambaye anakipiga katika klabu ya Besiktas kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Liverpool, amekanusha taarifa za kwamba mteja wake huyo anatarajia kuvunja mkataba na uongozi wa Besiktas. Tottenham KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Dele Alli, ameweka wazi kuwa, ana furaha kuongeza mkataba wa muda mrefu ndani ya klabu hiyo. Mchezaji huyo juzi alisaini mkataba wa miaka sita ambao utamfanya awe hapo hadi 2024.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.