Wakuu wa magereza mikoani wapanguliwa

Mtanzania - - Leo Ndani - NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

KAMISHNA Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi kwa kuwateua wakuu wa magereza wapya katika mikoa 19 Tanzania Bara (RPOs) na saba kuwabakiza katika nyadhifa zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja, Kasike ameteua maofisa sita kuwa wakuu wa vyuo vya magereza na kuwabadilisha maofisa watatu ndani ya jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, kwa mara ya kwanza, amewateua wakuu wa magereza wa mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa magereza katika ngazi ya mikoa hiyo.

“Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (Dar es Salaam) SACP Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Julius Ntambala, SACP Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake.

“Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA.

“Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi na nafasi yake inachukuliwa na ACP Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza.

“Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora.

“ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP Rymond Mwampashe.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo, akipokea hundi ya Sh milioni 16 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watoto mapacha waliotenganishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hivi karibuni, kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka (kulia).Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru na katikati ni wazazi wa watoto hao Dar es Salaam jana. – PICHA:DEUS MHAGALE

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.