Ali Kiba kudhamini Wasa¿ Festival

Mtanzania - - Leo Ndani - Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

MSANII nyota wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’, ameonyesha nia ya kutaka kudhamini tamasha la muziki la Wasafi Festival, linaloandaliwa na kundi Wasafi kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliweka wazi nia hiyo mara baada ya Mkurugenzi wa WCB, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz), kueleza wazi nia ya kumwalika tamasha la shoo ya Wasafi Festival, ambayo inatarajiwa kufanyika Novemba 24. Ali Kiba alifanya uzinduzi wa kinywaji chake cha Mo Faya tangu Mei mwaka huu, lakini kinywaji hicho kilikuwa bado hakijaanza kupatikana madukani. “Nashukuru sana kwa mwaliko wenu, ila kwa bahati mbaya sitaweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi nyingine. “Hata hivyo, tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa sapoti ya kudhamini tamasha lenu kupitia Mo Faya ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Afrika, uongozi utaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa,” alisema Kiba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.