Mbunge ataka vyombo vya kisasa vya uokoaji

Mtanzania - - Mkoa -

MBUNGE wa Nungwi, Yussuf Haji Khamisi (CUF), amehoji wa kuleta vyombo vya kisasa vya uokoaji kufuatia ongezeko la ajali za majini.

Pia amehoji Serikali inatoa tamko gani kuhusiana na watendaji wa bandarini ambao wamekuwa ni wazembe katika utendaji kazi wao.

Akiuliza swali jana bungeni, Khamis alihoji Serikali ina mpango gani wa kuleta vyombo vya kisasa vya uokoaji

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atastasta Nditiye,alisema kwa sasa kuna ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri wa majini katika maeneo mbalimbali.

Katika swali la msingi Khamis, alihoji Serikali ina mikakati gani endelevu kuhakikisha usafiri wa majini ni salama kwa maisha ya Watanzania. Akijibu, Nditiye alisema Serikali inatambua changamoto hizo na itazifanyia kazi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.