Magonjwa ya ngozi yan ayorithiwa kizazi kimoja hadi kingine

Mtanzania - - Jamii Na Afya - Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

NGOZI ni kati ya viungo muhimu katika mwili wa binadamu na ndicho ambacho kwa sehemu kubwa hufunika viungo vingine vya mwili. Kazi kubwa ya ngozi ni kuulinda na kuukinga mwili dhidi ya maambukizi mbalimbali, kuumia au hata kuungua na kemikali.

Husaidia mwili kuhisi joto, baridi, mitetemo, maumivu na hisia nyinginezo nyingi, huzalisha na kuhifadhi vitamin D na husaidia kutoa taka mwilini kwa njia ya jasho.

Kiungo hicho husaidia kuingiza virutubisho na dawa zinazotumika kutibu mwili kwa njia ya kupaka au kuchua, vile vile hufanya kazi ya kuzuia maji yasiingie ndani ya seli za mwili.

Hizo ni baadhi tu ya kazi za ngozi ambayo kibaiolojia imeundwa katika matabaka (layers) kuu tatu ambazo ni ngozi ya ndani kabisa (Hypodermis), ngozi ya katikati (Dermis) na ngozi ya nje au juu (Epidermis).

Yenyewe ina sifa ya kuwa na vitundu vidogo vidogo ambamo vinyweleo hujitokeza kupitia hapo.

Vinyweleo hivyo ndivyo ambavyo husaidia binadamu kuhisi na kutoa taka (jasho) mwilini mwake.

Ngozi kama ilivyo kwa viungo vingine vya mwili nayo huathiriwa na magonjwa mbalimbali na hivyo kuhitaji matibabu sahihi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician) wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Grace Shayo, anasema matibabu dhidi ya magonjwa ya ngozi hutegemeana na aina ya ugonjwa anaougua muhusika.

“Si magonjwa yote ya ngozi ambayo mtu hupata kwa kuambukizwa na mtu mwingine anayeugua kama ambavyo wengi hudhani, yapo baadhi ya magonjwa ya ngozi ambayo mtoto hurithi kutoka kwa wazazi wake. Kinachotokea Dk. Shayo anasema hali hiyo huweza kutokea pale ambapo mzazi mmoja au wote wawili wanakuwa wamebeba vinasaba ambavyo vinaweza kumuathiri mtoto anayeumbwa.

“Magonjwa ya ngozi ya kurithi yapo mengi, unakuta mzazi amebeba vinasaba ambavyo vinaweza kuleta tatizo la ngozi kwenye maisha ya mtoto wake. Yawezekana kabisa mzazi huyu anayemrithisha mwanawe vinasaba hivi vya matatizo ya ngozi hana kabisa tatizo hilo ingawa amebeba vinasaba vya tatizo au naye ni muathirika wa tatizo hilo.

“Kwa mfano, tunapozungumzia ‘albinism’ (watu wenye ulemavu wa ngozi), mzazi mwenyewe anaweza asiwe albino lakini mwili wake umebeba vinasaba vya ualbino.

“Ikiwa mwenza wake naye amebeba vinasaba hivyo, kuna uwezekano wakazaa mtoto albino, ndiyo maana unaweza kukuta baadhi ya familia zina watoto albino lakini wazazi wao si albino,” anabainisha.

Anaongeza “Hiyo inatokana na mfumo

ule wa urithishwaji wa vinasa vipo vinasaba ambavyo ukirit kimoja tu (kwa mzazi mmoja linaweza kutokea kwa mtoto.

“Kitaalamu hiyo tunaita ‘A Dominant Inheritance’ ina m kile kinasaba kimoja chenyew na mamlaka na nguvu ya kuw bisha tatizo kutokea.

“Mfumo mwingine wa ur huusisha vinasaba dhaifu (Au cessive Inheritance) ambavyo mzazi achangie kinasaba cha mtoto ili tatizo litokee.

Mfano wa urithishwaji hu albinism ambapo wazazi wot pasisha kinasaba kwa mtoto a na albinism. Lakini kama mza ana vinasaba vya albinism na wake hana kabisa, watoto wat hawatakuwa albino lakini kun watarithi kile kinasaba nao w kwa vizazi vyao. Magamba kama nyoka “Kuna ugonjwa wa ngozi taalamu Ichthyosis vulgaris. na mengine mengi ya jamii y kana na hali ya kulimbikizwa cha ngozi kiitwacho keratin k la juu la ngozi hivyo kupeleke na mpasuko wa ngozi unaofa ifanane na ngozi ya nyoka au aliyeparuliwa magamba yake. jamii yake hutokana na maba vinasaba fulani ambavyo hue wa ngozi.

Tatizo hili huwaathiri zaid kuanzia miaka 3 -12 lakini pia kwa watu wazima na huhusis magaga ya nyayoni), mikono, fua, mgongo na uso na kuach mikunjo ya mwili kama nyum

na viwiko vya mikono (elbows).

Ifahamike kuwa karibu kila tatizo la ngozi litasababisha hali ya magamba magamba, hivyo ni muhimu muhusika kuchunguzwa hospitalini ili kujua kwa uhakika tatizo alilo nalo.

Katika kundi la magonjwa haya ya ulimbikizwaji wa keratin kuna tatizo linaitwa keratosis pilaris ambalo linasababisha ulimbikizwaji wa keratin na kufanya ngozi kuwa rafu kama msasa wa mbao.

Nalo hili huathiri zaidi watoto. “Ninapokea wagonjwa wengi hasa watoto ambao huja na tatizo hili, vipele vinakuwa vikali ukivigusa kama vile msasa ule unaotumika kusugua mbao,” anabainisha

Anaongeza; “Lakini kuna aina fulani mbaya zaidi ya ulimbikizwaji wa keratin inaitwa Harlequin ambayo mtoto hurithi na anazaliwa akiwa na ngozi imepasuka pasuka, na wengi hufariki dunia saa chache baada ya kuzaliwa.

“Kwa sababu hutoka akiwa anavuja maji maji ya mwili toka kwenye mipasuko ya ngozi ni rahisi kupoteza maji mengi ya mwili na kupata maambukizi ya bakteria katika mipasuko hiyo hivyo, kusababisha kifo siku chache au miezi michache baada ya kuzaliwa ,” anasema. “Sugu” Dk. Shayo anasema upo ugonjwa mwingine wa ngozi uitwao kitaalamu Palmoplantar keratoderma ambapo mtu hupata vitu kama sugu kwenye vitanga vya mikono na nyayo zake.

“Sugu” hizo zinakuwa na maumivu makali sana hasa zile za kwenye nyayo (Si sugu za kawaida zinazopatikana kwenye vidole). Kucha kubanduka Daktari huyo anataja ugonjwa mwingine wa ngozi wa kurithi unaitwa kitaalamu Psoriasis, huu ni ule ukuaji usio wa kawaida wa seli za ngozi hivyo kujilimbikiza katika tabaka la juu la ngozi.

“Kutokana na hali hiyo, huathiri ngozi, kucha na maungio ya mifupa (joints). Magamba yake ni ya rangi ya fedha na makavu hivyo hufananishwa na ulanga (Mica). Magamba haya hutoka kwa urahisi na mara nyingi hukutwa yametapakaa kitandani kwa mgonjwa. Kama sehemu kubwa ya mwili imeathiriwa na hali hiyo, hutoa magamba mengi na kama yatakusanywa basi yanaweza hata kujaa kwenye kontena ya ujazo wa lita mbili au zaidi.

“Kuna watu ambao huathiriwa kwenye kucha tu, unakuta imetengeneza vishimo vidogo vidogo na chini yake kunakuwa na magamba mengi. Kucha hubanduka kutoka kwenye ngozi ya kidole karibu nusu nzima ya sehemu ya mbele kutoka kwenye ncha ya kidole.

“Mtu anaweza akawa na maumivu makali ya viungo (joints), anaweza akaona dalili zote kwa pamoja pia yaani magamba kwenye ngozi, mabadiliko ya kucha na maumivu ya viundo au anaweza akawa na kimojawapo,” anasema. Anasema hali hiyo hutokana na hitilafu tu ya mfumo katika ‘chromosome’ za mwili wake na kwamba kucha inaweza kubanduka pasipo kuoza. Kuna tofauti kubwa ya kucha yenye maambukizi ya fangasi na ile yenye psoriasis. Pumu ya ngozi (Eczema) Anasema ugonjwa mwingine wa ngozi wa kurithi unaitwa kitaalamu Eczema, ni tatizo sugu ambalo huwapata zaidi watoto hasa katika kipindi cha mwezi mmoja hadi wa tatu tangu kuzaliwa lakini pia huweza kumuatiri mtu kwenye umri wowote.

Eczema inaitwa pumu ya ngozi kwa vile ipo kundi la magonjwa yanayoitwa atopy pamoja na pumu ya mapafu na aina fulani ya mzio unaosababisha mafua ya mara kwa mara, kuwashwa macho na koo.

“Watoto wadogo wenye eczema huonesha hali za matatizo ya ngozi kwenye uso hasa shavuni. Wanapokua kidogo tatizo hujidhihirisha zaidi maeneo yenye mikunjo kama shingoni, viwiko vya mikono na nyuma ya magoti lakini yaweza tokea sehemu yoyote.

“Hali hii hutokea ikiwa kuna uharibifu katika kinasaba kinachosimamia utengenezwaji wa vilainishi asilia vya ngozi (Filaggrin) na kutetereka kwa uwezo wa ngozi kujikinga.

“Ngozi yenye afya yaweza kudumu muda mrefu bila kuhitaji kupakwa mafuta kwa sababu ya uwepo wa hiyo kemikali, lakini isipokuwepo ngozi ya muhusika huathirika,” anabainisha. Lehamu (cholesterol) kwenye damu “Tatizo jingine la ngozi la kurithi linaitwa Familial Hypercholesterolemia, ni ile hali ambayo unakuta kiwango kikubwa cha lehamu (cholesterol) kwenye damu kuliko kawaida.

“Kuna watu wanarithi hili tatizo toka kwa wazazi wao. Wingi wa lehamu husababisha athari mbalimbali si tu kwenye mishipa ya damu bali hata kwenye ngozi.

“Lehamu hulimbikizwa kwenye maeneo maalumu ya ngozi kama vile kwenye kope za juu na chini za macho upande wa pua, huweka mabaka ya rangi ya njano sehemu hizo. Lehamu pia yaweza limbikizwa kwenye kwenye sehemu ya mwisho ya misuli ya mwili ambayo hushikiza kwenye mifupa, unakuta mtu nyuma ya kisigino au kwenye magoti kuna nundu kadhaa, Uvimbe katika mfumo wa neva wa ngozi Dk. Shayo anataja ugonjwa mwingine kitaalamu ni neurofibromatosis. Hii ni hitilafu katika seli za neva inayosababisha kuota vivimbe vingi katika ngozi.

Vivimbe hivi huendelea kukua na vyaweza kusababisha ngozi kuninginia. Kwa mfano kope ya juu ya jicho yaweza kunin’ginia mpaka kwenye bega na kufunika jicho kabisa. Hali hii inaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili.

“Uvimbe huo huanza kidogo kidogo na hatimaye kuwa mkubwa sana kiasi cha mgonwja kuhitaji kufanyiwa upasuaji kuuondoa,” anabainisha.

Uning’iniaji huu huonekana zaidi katika aina ya kwanza ya neurofibromatosis. Aina ya pili ya neurofibromatosis huwa na uziwi zaidi na matatizo ya kupoteza uoni kwa ajili ya athari katika masikio na macho. Wagonjwa wa neurofibromatosis huwa kwa kawaida wana kimo kifupi, kichwa kikubwa kuzidi watu wengi wanaowazunguka, matatizo ya mifupa na wengine hupata shida ya uelewa darasani. Ehlers - Danlos syndrome Anasema katika jamii wapo watu ambao ngozi zao huvutika sana na viungo vyao huwa laini kuliko kawaida, hawa wana tatizo la ngozi liitwalo kitaalamu Ehlers-Danlos syndrome.

“Unakuta anaweza kuivuta ngozi yake na ikavutika sana, hali hii huweza kuathiri pia viungo vingine vya mwili ikiwamo mishipa ya damu na mfumo wake wa chakula,” anasema.

Hata hivyo anasema ingawa yapo magonjwa ya ngozi ambazo sababu zake hujulikana lakini yapo pia magonjwa mengine ya ngozi ambayo hutokea na sababu zake hazijulikani. Matibabu Anasema matibabu dhidi ya magonjwa ya ngozi ya kurithi hutegemeana na aina ya ugonjwa wa ngozi anaougua mgonjwa husika.

“Kuna ambao huhitaji upasuaji, dawa za kutuliza maumivu au kupunguza ukali wa tatizo. Hizi zinaweza kuwa za kumeza, sindano au za kupaka.

“Kuna wanaohitaji kutegemezwa waweze kuishi na tatizo lao kwa hali bora zaidi.

“Lakini utaona sasa hivi kuna tafiti nyingi zinaendelea, watafiti wanajaribu kuvumbua dawa zitakazosaidia kufanya marekebisho katika vinasaba vya wagonjwa mbalimbali.

“Huu ni muelekeo mzuri hasa katika kutafuta matibabu ya magonjwa haya ya kurithi,” anabainisha.

Daktari Bingwa wa Magonj

wa ya Ngozi MUHAS, Grace Shayo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.