Maktaba kwa wanafunzi

Mtanzania - - Kanda -

WALIMU wa wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza wameshauriwa kuanzisha maktaba katika shule zao kuwajengea maarifa ya kusoma vitabu mbalimbali, anaripoti Sheila Katikula.

Wito huo ulitolewa juzi na Ofisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Mwanza, Sheja Josephat katika maadhimisho ya Wiki ya Msomaji kupitia mradi wa kusoma, kuandika na kuhesahu katika maktaba ya Mkoa wa Mwanza.

Alisema iwapo kukiwa na maktaba katika shule mbalimbali kutachochea ari ya kujisomea na kujenga tabia ya wanafunzi kujisomea.

Alisisitiza kuwa maktaba husaidia kuchochoea kiwango cha wanafunzi kujua kusoma, kuhesabu na kuandika.

Mkutubi wa Maktaba ya Mkoa wa Mwanza, Velda Kuboja alisema maktaba za umma ndiyo mahali pekee ambako kunahifadhiwa machapisho ya aina mbalimbali yenye maarifa na kumwezesha mtoto au watu wanaopenda kusoma kutambua mambo mengi bila kujali jinsia, umri na kiwango cha elimu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.