Ucheleweshaji miradi ya maji unavyowagharimu wananchi

Mtanzania - - Jamii Na Afya - Na MWANDSHI WETU -MANYARA

TAFITI zinaonyesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na rasilimali za maji juu ya ardhi zenye kilomita za ujazo 92.27 na chini ya ardhi kilomita za ujazo 38. Kupitia rasilimali hii lengo la Serikali ni kuhakikisha wakazi wa vijijini wanapata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 95 itakapofika mwaka 2020. Serikali imeweka nguvu kubwa katika kuhakikisha wananchi ambao ndio wadau wake wakuu wanapata huduma hii muhimu ya majisafi na salama karibu na makazi na si kutembea umbali mrefu.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu, ambaye asilimia 63 ya wakazi wa wilaya anayoiongoza wanapata majisafi na salama anasema moja ya changamoto katika miradi ya maji ni uvamizi na uchafuzi wa vyanzo vya maji.

Wastani wa upatikanaji maji mjini Babati utaongezeka siku za usoni na kufikia asilimia 95 baada ya mradi wa maji wa Bonga unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Babati (BAWASA) kukamilika.

Mradi huo utazalisha lita 40,000 kwa saa moja. Vijiji vya jirani vitaunganishwa katika mradi huo.

Diwani wa Minjingu, Michael Milao, anasema jambo la msingi ni kwa watalaam kuwashirikisha wananchi katika masuala ya maji.

Anasema kutokuwa na elimu na taarifa za kutosha kunasababisha baadhi ya wananchi kufanya mambo wanavyoamini.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Tsamas, Jumanne Selemani, anasema kutoshirikishwa kwa wananchi na kupewa elimu ni tatizo.

“Hawawezi kukabidhiwa mradi tu bila kushirikishwa toka mwanzo na kujua mbinu za utunzaji vyanzo vya maji,” anasema Selemani.

Shughuli za kibinadamu zinasababisha kwa kiwango kikubwa vyanzo vya maji kukauka kabisa au kutoa maji kwa msimu. Kwa mfano, mkoa wa Manyara vyanzo vyake vikuu vya uchumi ni kilimo na ufugaji kwa kuajiri asilimia 83 ya wakazi.

Shughuli nyingine zimeajiri asilimia 17 ikiwamo utalii, uchimbaji madini, uvuvi, biashara, viwanda vidogo na kazi za ofisi.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akizungumza na wakazi wa Waranga, Katesh anasema ni jambo la msingi kulinda vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa huduma endelevu ya majisafi na salama.

Wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Katesh uliofanikishwa na BAWASA, alisema hatamvumilia mkandarasi anayedanganya wananchi kwa kuweka miundombinu ya maji wakati hajafanya utafiti wa kina kupata chanzo cha maji cha uhakika.

Mradi wa Katesh unatarajia kutoa huduma kwa miaka 20 ijayo kwa wakazi 40,000 na una visima vinavyotoa lita za maji 150,000 kwa sasa.

Anasema hadi Septemba 2018 katika Mkoa wa Manyara upatikanaji wa maji vijijini ulikuwa asilimia 52 na Babati mjini asilimia 75, wakati mkoa huo una vyanzo vya maji mbalimbali ikiwamo visima virefu 296, visima vifupi 320, chemchemi 93 na mabwawa 123.

Wakati wa ziara ya mradi kwa mradi, Naibu Waziri huyo alibaini baadhi ya vyanzo vya maji kuvamiwa kwa shughuli mbalimbali, ikiwamo kilimo, ufugaji na kazi za kufyatua matofali hali inayohatarisha upatikanaji wa maji kuwa endelevu.

Aliwaelekeza viongozi na wananchi mkoani Manyara kulinda na kuelimisha kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwa maendeleo ya kila mwananchi.

“Hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji, kila mkazi wa Manyara anatakiwa aelewe,” anasema Aweso.

Akiwa katika mradi wa maji wa Gehandu mkoani Manyara aliwaelekeza watalaam wa maji kote nchini kuacha mara moja kuweka miundombinu ya maji wakati bado hawajatafiti kupata chanzo cha uhakika cha maji.

“Ni ubabaishaji, si weledi bali kuchezea rasimali za wananchi, na wakati huduma ya majisafi

Inaendelea uk. vi

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiangalia maji yanayochotwa katika Mto Tsamas kwa matumizi mbalimbali ya wananchi, maji hayo si salama.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.