Ucheleweshaji miradi ya maji unavyowagharimu wananchi

Mtanzania - - Jamii Na Afya -

hawapati pamoja na gharama kubwa kutumika kuweka miundombinu ambayo inakosa maji,” anasema.

Pia, alimwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ kuwahoji wate

waliohusika na mradi wa maji wa Gehandu kwa sababu ya makosa mbalimbali ya kitalaam na atayeonekana kuhujumu mradi achukuliwe hatua za kisheria.

Anasema haiwezekani mtaalam aruhusu malipo kwa mkandarasi aliyefanya kazi kijanja na mkandarasi huyo ametakiwa kurudi katika eneo la mradi mara moja.

Naibu Waziri huyo pia aliwaelekeza wataalam wa rasilimali maji kanda ya kati kwenda katika eneo la Gehandu, wilayani Hanang’ na kufanya utafiti ili kupata chanzo cha maji cha uhakika chenye maji ya kutosha.

Aweso anasema wananchi hawawezi kukaa kusubiri mradi wa maji kwa muda mrefu kiu yao ni maji si maneno.

Akihutubia wananchi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika viwanja vya CCM Dongobesh na Uwanja wa Ofisi ya Kata ya Haydom, Aweso anasema timu ya watalaam wa maji kutoka Wizara ya Maji itatumwa mara moja kuchunguza miradi yote ya maji mkoani Manyara.

Moja ya mradi ulioonekana kukosa utalaam ni mradi wa maji Darakuta – Minjingu uliosanifiwa mwaka 2009 ambao wananchi wamelalamika mabomba yaliunganishwa kwa kutumia sabuni.

Aidha, mabomba yaliyopita ziwani yameachia, hivyo lengo la kufikisha maji kwa wananchi kutotimia.

Katika mkutano uliofanyika Wilaya ya Simanjiro, Aweso ameelekeza mkandarasi aliyejenga mradi wa maji wa Olbil - maarufu kama mradi wa vijiji 10, unaotarajiwa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 7500, kurudia kazi ya kuchimbia miundombinu ya maji kwa gharama zake.

Hiyo ni baada ya wananchi kupaza sauti kuwa katika mradi huo mabomba yamefukiwa juu na mvua iliyonyesha wakati wa mkutano ilihdihirisha hilo baada ya mabomba kuibuka kutokana na kufukiwa kwa kina kifupi.

Miundombinu hiyo ya maji imewekwa kwa thamani ya Sh milioni 312 fedha iliyotolewa na Serikali.

Katika kuhakikisha majisafi na salama yanawafikia wananchi wa Simanjiro mkoani Manyara, Aweso ametaka Wakala ya Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) kukamilisha kazi ya majaribio ya pampu katika mradi wa maji Mirerani.

Hatua hiyo itasaidia kujua kiwango na ubora wa maji kabla hayajasambazwa kwa wananchi. Kukamilika kwa kazi hiyo kutafuatiwa na hatua ya usanifu wa mradi itakayofanywa na BAWASA.

Naye Ofisa Rasilimali maji kutoka Bonde la Kati, Lazaro Msengi, anasema kila mwananchi anatakiwa kuelewa kuwa maji ni uhai, lazima kutunza vyanzo hivyo na kuvilinda kwa kuweka mipaka ili kuepuka shughuli za aina yoyote katika maeneo hayo.

“Pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, rasilimali maji inaisha kwa kasi ya kutisha. Hivyo, mkiendelea kuingiza mifugo katika vyanzo vya maji na kulima mazao, ni dhahiri kuwa haitachukua muda mrefu mtaomba huduma ya majisafi na salama wakati vyanzo vya kutoa maji hayo mmeshavimaliza wenyewe kwa tamaa ya kufuga mifugo au kufanya kazi za kilimo,” anasema Msengi.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, Joseph Mkirikiti, ameagiza shughuli zote katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 zikome mara moja.

Akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika katika mradi wa maji Endasaboghechan na Waranga, anasema fedha za serikali zinazotumika katika miradi ya maji ni kubwa, na hawezi kuvumilia kumuona mtu anaingia katika chanzo cha maji kwa tamaa ya kulima au kufanya kazi yoyote.

“Mwananchi anayejua yupo ndani ya chanzo cha maji, kwa kuweka mifugo, kufyatua matofali au kilimo awe amejiondoa mwenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu,” anasema Mkirikiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa BAWASA, Mhandisi Yazidi Msuya, anasema ni vizuri wataalam wakashirikiana kuondoa makosa ya kitalaam na kukamilisha miradi mapema zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.