Wanafunzi 79 waliotekwa waachiwa Cameroon

Mtanzania - - Kimataifa - YAOUNDE, CAMEROON

WANAFUNZI 79 waliokuwa wametekwa na watu wenye silaha mapema wiki hii katika eneo linalozungumza Kiingereza la hapa wameachiwa.

Waziri wa Mawasiliano, Issa Bakary Tchiroma alisema jana kuwa wanafunzi wote 79 wameachiwa bila kutoa maelezo ya namna walivyoachiwa.

Utekaji nyara huo uliotokea Jumatatu wiki hii, ulikuwa tukio la kwanza kubwa kushuhudiwa nchini hapa na limetokea kipindi ambacho kuna hali tete kisiasa katika taifa hili, ambalo kwa sehemu kubwa linazungumza Kifaransa.

Wanafunzi hao wanasoma Shule ya Sekondari Presbyterian huko Bamenda, mji mkuu wa Eneo la Kaskazini Magharibi ya Cameroon, moja ya maeneo mawili waishio wanaozungumza Kiingereza, ambako wanamgambo wanaotaka kujitenga wanakabiliana vikali na majeshi ya Serikali.

Kuachiwa kwao kunakuja siku moja baada ya Rais Paul Biya (85) kuapishwa kwa muhula wa saba madarakani.

Biya ameahidi kuendeleza sera ya ugatuzi wa madaraka ili kukabiliana na hali ya kukata tamaa na kutimiza matakwa ya maeneo yazungumzayo Kiingereza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.