Mapambano yapamba moto Hodeida

Mtanzania - - Kimataifa - SANAA, YEMEN

WANAJESHI wa Serikali na waasi wamepambana tena karibu na mji wa Bandari wa Yemen, Hodeida, ambao ni muhimu katika upitishaji wa msaada wa kibinadamu.

Siku tano za mapambano kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na jeshi la hapa linalosaidiwa na jeshi la ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia, zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 150 katika mkoa wa Bahari ya Sham wa Hodeida.

Msemaji wa jeshi la ushirika alisema hawana mipango ya kufanya mashambulizi kamili ya kuukomboa Hodeida.

Lakini maofisa kadhaa wa kijeshi kwenye eneo hilo waliripoti kuwa wanajeshi wao wameuzingira mji huo unaodhibitiwa na waasi.

Mapigano hayo yanakuja wakati Umoja wa Mataifa ukishinikiza kuanzishwa tena kwa mazungumzo kati ya pande zinazozozana, baada ya mazungumzo ya awali kuvunjika jijini Geneva, Uswisi Septemba mwaka huu.

Hodeida ni mojawapo ya ngome za mwisho za Wahouthi katika mwambao wa magharibi mwa Yemen.

Waasi hao waliikamata bandari hiyo na mji mkuu mwaka 2014.

Jeshi linaloongozwa na Saudia linaloshirikisha Umoja wa Falme za Kiarabu limezikomboa bandari kadhaa za nchi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.