Afya kwa wananchi

Mtanzania - - Kanda -

WANANCHI Wilaya ya Maswa wameiomba serikali, wadau wa afya na mashirika binafsi kujitokeza kwa wingi kusaidia kutoa huduma za afya kuwasaidia kuepukana kuifuta huduma hiyo umbali mrefu, ANARUIPOTI SAMWEL MWANGA.

Baadhi ya wananchi walikuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika Mji wa Malampaka wilayani humo juzi katika kampeni ya kutoa huduma za afya iliyotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Walisema mfuko huo umewasaidia kuwasogezea huduma za afya na kuomba iwe endelevu.

Rahel Charles mkazi wa Kijiji cha Malampaka, alisema huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa kina mama wanazipata kwa kutegemea Hospitali ya Wilaya ya Maswa umbali wa kilomita 30 na husafiri zaidi ya saa mbili kwa baiskeli ili kuipata.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.