Mradi wa mazingira

Mtanzania - - Kanda -

SERIKALI ya Marekani imetoa Sh bilioni 20 kwa Taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na utafiti wa sokwe mkoani Kigoma kuboresha mazingira ya uhifadhi kwenye mikoa ya Katavi na Kigoma hivyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ANARIPOTI MUSSA BUNDALA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano na Mazingira, January Makamba alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi katika mikoa ya Katavi na Kigoma uliofanyika mjini Kigoma juzi.

Alisema fedha hizo zitatumika kwa miaka mitano kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uhifadhi mazingira kwa lengo la kuleta mabadiliko makubwa kwa mikoa husika.

Makamba alisema serikali inaunga mkono mradi huo kwa asilimia kubwa kutokana na tasisi inayoutengeneza ya Jane Goodall Institute kutekeleza kwa kuwashirikisha wananchi wanaozunguka mradi hali ambayo huondoa migogoro kati ya tasisi na jamii.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk. Carlos Drews alisema mradi huo utalenga kutoa elimu ya afya, utawala bora katika mikoa hiyo hali ambayo itawajengea jamii uelewa wa masuala ya uhifadhi wa mazingira ikiwamo ardhi na misitu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.