Mbunge ashauri watoto waliotelekezwa waasiliwe

Mtanzania - - Kanda -

MBUNGE wa Viti Maalum, Fatma Toufiq (CCM) amehoji Serikali haioni umuhimu kuwaasili watoto waliotelekezwa.

Akiuliza swali bungeni jana,Toufiq alisema watoto wengi wametelekezwa na wazazi wao na kuachwa wakizagaazagaa mitaani.

“Je,Serikali haioni kuwa sasa umefika wakati kuhamasisha jamii kuwaasili watoto hao ili nao wafaidike na malezi ya jamii,”aliuliza Toufiq.

Akijibu kwa niaba ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,JinsiaW, azee na Watoto, Dk.Hamisi Kigwangala alisema matunzo na ulinzi wa mtoto ni haki ya mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.

Dk.Kigwangala ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kifungu cha 8 na 9 kinatoa majukumu kwa mzazi ama mlezi na mtu yeyote mwenye jukumu la kumlea mtoto kuhakikisha anawatunza ipasavyo watoto wake ikiwamo kuwapatia huduma za msingi kama chakula,malazi,mavazi na elimu.

Alisema kifungu cha 14 cha sheria ya mtoto kinatoa adhabu kwa mlezi ama mzazi yeyote atakaekiuka kifungo hicho kutozwa faini isiyizidi Sh milioni tano au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.

Alisema kwa mujibu wa taarifa ya utafiti ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ya mwaka 2018, watoto 6,393, wanawake 1,528 na wanawaume 4865 walitambuliwa katika mikoa sita.

Dk.Kigwangala aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Mwanza.

Alisema hadi kufikia Juni 2018, watoto 1,745 walikuwa wamepatiwa huduma mbalimbali kama vile kuunganishwa na familia zao,kurudishwa shuleni kupatiwa stadi za maisha na kuanzisha vikundi vya ujasiriamali.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wanaunganishwa na familia wapate huduma zote za msingi ikiwamo haki ya kulelewa na kutunzwa katika familia,”alisema.

Dk.Kigwangala alisema Serikali imeendelea kutoa uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuasili watoto kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kupitia maadhimisho ya kitaifa ya siku ya mtoto,”alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.