Mchezaji wa kikapu Tanzania apata dili Canada

Mtanzania - - Michezo - Na DAMIAN MASYENENE

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 18 ya mchezo wa mpira wa kikapu, Atiki Ally, amepata ufadhili wa kusoma nchini Canada.

Atiki, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Highview ya Dar es Salaam, alikokuwa akisoma kwa ufadhili wa mchezo wa kikapu, anatarajiwa kwenda nchini Canada, ambako atendelea na masomo yake katika Shule ya Themes Valley District School Board.

Mchezaji huyo amewahi kuchezea timu za JMK Park Academy, Jogoo, pia aliweza kushiriki mafunzo maalumu ya mpira wa kikapu kwa vijana nchini Afrika Kusini, yaliyosimamiwa na NBA, akiwa miongoni mwa wachezaji 50 bora kutoka Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA), kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na Uendeshaji, Haidari Abdul, mchezaji huyo amepata ufadhili huo kupitia Juco Advocates, waliokuja nchini kwa mwaliko wa kocha wa timu ya Taifa, Matthew McAllister, Agosti, mwaka jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.