Basata yataka wanaocheza na fisi, nyoka kupata vibali

Mtanzania - - Burudani - Na HARRIETH MANDARI

BARAZA la Sanaa Tanzania (Basata), limewataka wasanii wa ngoma za asili wanaotumia wanyama wakiwemo nyoka na fisi kufuata utaratibu wa kupata kibali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya umiliki na kuwatumia wanyama hao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano, uliojumuisha maofisa utamaduni kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa uliofanyika mjini Geita juzi, Ofisa Habari Mkuu wa Basata, Agnes Kimwaga, alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa sheria baada ya maofisa utamaduni kuwasilisha malalamiko, wanayopata kutoka kwa wasanii juu ya mlolongo mrefu wa kupata kibali hicho.

“Kiutaratibu msanii anatakiwa aende wizara ya maliasili ili kupata kibali, vinginevyo ni kukiuka sheria hivyo nawakumbusha wasanii kufuata utaratibu, nina uhakika wakifuatilia kibali watapata tu,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.