Utafiti: Uvutaji sigara huongeza hatari kwa wanawake kupata mshtuko wa moyo

Mtanzania - - Habari -

WANAWAKE wanaovuta sigara, wanaougua kisukari au wenye tatizo la shinikizo la damu wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa Uingereza, wanawake wanastahili kupewa ushauri sawa na wanaume na pia kupewa ushauri wa kuachana na uvutaji sigara.

Umetoa wito kwa madaktari kusaidia katika harakati ya kuwatambua wanawake walio katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo.

Hata hivyo, watafiti hao wanasema wanaume bado wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo mara tatu zaidi ya wanawake.

Utafiti huo uliofanywa na watafiti wa Chuo Hikuu cha Oxford ulijumuisha karibu watu 500,000 wenye umri wa miaka kati ya 40-69 ambao wameorodheshwa katika takwimu za afya za Uingereza.

Watafiti walibaini kuwa watu, 5,081 waliofanyiwa uchunguzi walikabiliwa na mshtuko wa moyo zaidi ya miaka saba na wengi wao ni wanawake. Ingawa hatari ya kupata mshtuko wa moyo kwa wanawake iko chini kuliko wanaume wa miaka yote, kuna baadhi ya sababu zinazowafanya wawe katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo. Wanawake wanaovuta sigara wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo kuliko wale ambao hawavuti sigara. Wanaume wanaovuta sigara wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo mara mbili zaidi.

Shinikizo la damu linaongeza hatari ya wanawake kupata mshtuko wa moyo kwa asilimia 83.

Utafiti pia umebaini kuwa aina ya kwanza na ya pili ya kisukari zinawaweka wanawake katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo kuliko wanaaume

Watafiti wanasema sababu za kibayolojia huenda zikachangia hali hiyo.

Kwa mfano aina ya pili ya kisukari, ambayo mara nyingi inahusishwa na mtindo wa maisha ya mtu binafsi huenda ikaathiri zaidi moyo wa mwanamke kuliko ule wa mwanamume.

Hata hivyo, utafiti unasema wanawake hawana ufahamu kuwa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na huenda wakawa wanapokea matibabu yasiyofaa.

Watafiti wanasema wanaume pia huenda wakawa katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo lakini ugonjwa huo umechangia kwa kiasi kikubwa vifo vya wanawake nchini Uingereza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.