Waziri Mbarawa awa ‘mbogo’ kwa Dawasa

Mtanzania - - Habari - NA TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, amesema hatasita kuwachukulia hatua za nidhamu mara moja mameneja na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) kwa kushindwa kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya kata za Tabata na Bonyokwa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam, Mbarawa aliwaonya watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wajipange upya kuwahudumia wananchi.

Alisema yamekuwapo malalamiko mengi ya wateja wa maji kutokana na huduma wanazopata lakini hawapatiwi majibu wakati watendaji wapo.

“Watendaji na mameneja ambao hawataki kujifunza na kubadilika nitawachukulia hatua mara moja kama mlivyoona jana nimemchukulia hatua mmoja na wa hapa nimempa onyo lakini pia nimegundua utendaji wa watumishi wa Dawasa hauko vizuri na wanafanya kazi kwa mazoea,” alisema Profesa Mbarawa.

Katika ziara hiyo, Waziri Mbarawa alisema malengo waliyojiwekea katika kukusanya mapato ya Dawasa hayakufikiwa huku akiwatuhumu mameneja wa Kimara na Tabata kwa uzembe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.