FURSA ZA UWEKEZAJI NA UTALII KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA

Mtanzania - - Fursa, Uwekezaji Na Utalii Nyanda Za Juu Kusini -

Shamba la mpunga

HALMASHAURI ya wilaya ya Momba ni miongoni mwa Halmshauri 5 zinazounda Mkoa wa Songwe. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ilikuwa na jumla ya watu 168,739 ikiwa wanaume ni 80,785 na wanawake ni 87,954. Mwaka 2018 Halmashauri inakadiriwa kuwa na watu 198,269 kati yao wanaume ni 94,923 na wanawake ni 103,346. Kiwango cha ukuaji wa watu katika Halmashauri ni wastani wa 2.7% kwa mwaka na idadi ya kaya zilizopo katika vitongoji vyote ni 36,912.

JIOGRAFIA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA

Halmashauri ya wilaya ya Momba inapatikana katika latitudo ya 8010’ kusini na 90 15’’ Kusini mwa Ikweta na longitude ya 320 5’ Mashariki na 320 45’’ Mashariki mwa Greenwich ya Meridian. Halmashauri ipo katikati ya 900 mita hadi 2750 mita kutoka usawa wa bahari. Wastani wa mvua kwa mwaka ni 1,350 milimita hadi 1,550 milimita na joto linaanzia 200C hadi 280C. Halmashauri imepitiwa na bonde la Ufa ambapo limegawanya Halmashauri katika kanda mbili ambazo ni Ukanda wa juu na ukanda wa chini. Halmashauri ya wilaya ya Momba imepakana na Zambia, Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Mbozi na Songwe.Vilevile Halmashauri imepakana na Ziwa Rukwa ambapo limechukua ukubwa wa kilomita za mraba 292.

UCHUMI KISEKTA SEKTA YA KILIMO

Sekta ya kilimo ni moja ya sekta muhimu katika Halmashauri ya Momba kwa kuwa inatoa nafasi ya ajira kwa asilimia 90.3 kwa jamii. Mazao makuu ya chakula yanayostawi ni Mahindi, Mpunga, Mtama, Maharage, Viazi mviringo, Mhogo, Viazi vitamu, Mboga na Matunda, na mazao ya biashara ni Ufuta, Ulezi, Karanga na Alizeti. Halmashauri ina jumla ya ukubwa wa Hektari 562,404.2. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Ha 360,669.81. Kati ya hizo zinazolimwa ni takribani Hektari 100,700. Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hektari 56,400 na eneo linalomwagiliwa ni Hektari 5,000. Halmashauri ina nafasi kubwa ya uwekezaji upande wa kilimo pamoja na Masoko. katika Halmashauri hii kuna skimu moja ya umwagiliaji ya Naming’ongo ambayo inatumika katika umwagiliaji wa zao la mpunga, Ha 1500 za mpunga hulimwa katika skimu hii.

SEKTA YA UFUGAJI

Halmashauri ya Wilaya ya Momba ina wafugaji wenyeji na wafugaji wahamiaji kutoka Mikoa ya jirani kama Rukwa, Katavi, Tabora na mikoa ya Kanda ya Ziwa. Idadi ya Mifugo ya wafugaji wenyeji kulingana na takwimu zilizokusanywa na Maafisa Ugani kwa mwaka 2017/2018, wapo Ng’ombe 123,219, Mbuzi 73,497, Kondoo 9,884, Kuku 102,620 na Kanga 5,558. Jumla ya malambo 2 ya kijiji cha Kasanu na Mkomba yanatumika katika kunyweshea mifugo.

Vilevile Shughuli za uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya zinaendeshwa na wavuvi wapatao 532 katika Ziwa Rukwa lenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,101, kati ya hizo, kilomita za mraba 292 zipo katika Halmashsuri ya Wilaya ya Momba (sawa na asilimia 28.9).

SEKTA YA ELIMU

Halmashauri ya Wilaya ya Momba ina jumla ya Shule za Msingi 75 ikiwa shule zote ni za serikali. Kuna jumla ya Wanafunzi 47,110 ambapo kati yao 23,464 ni wavulana na 23,646 ni wasichana. Vilevile Halmashauri ya Wilaya ya Momba ina jumla ya shule za sekondari 9 ambapo shule hizo zina kidato cha I-IV. Idadi ya wanafunzi katika shule zote za sekondari ni 3,101 kati ya hao wavulana ni 1,786 na wasichana ni 1,315.

Hali ya ufaulu wa Mtihani wa kuhitimu darasa la saba 2018, Halmshauri ya wilaya ya Momba imeongoza katika Mkoa wa Songwe, kati ya Halmashauri tano (5) imekuwa ya kwanza (1) kwa kufaulisha wanafunzi.

MAENEO YA VIWANDA

Wilaya ya Momba imetenga jumla ya Ekari 253.015 kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda. Maeneo hayo yako katika kata tano(5) za Chitete, Ikana, Kamsamba, Nkangamo na Msangano kama ifuatavyo.

MALIASILI NA UTALII

Misitu ni mojawapo ya maliasili inayopatikana katika Halmashauri ya wilaya ya Momba. Zipo Hektari 134,058 za misitu ya asili ambapo Hektari 112,724 ni misitu ya kupandwa. Ipo misitu ya asili ambayo ina miti ya jamii inayofaa kwa ajili ya ufugaji wa Nyuki. Vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Halmashauri ya wilaya ya Momba ni uwepo wa Unyayo wa binadamu wa kale, Michoro juu ya mawe, Bonde la Ufa, Maporomoko ya maji, Ziwa Rukwa, Uwepo wa tamaduni za kimila za Kinyamwanga(CHIEF), Jengo la Kanisa la kale la Katoliki (1901), Uwepo wa Wanyama kama Kiboko na Mamba Ziwa Rukwa, Uwepo wa madaraja 14 ya asili ya kuning’inia(Kiteputepu) na Uwepo matanuru ya asili ya kutengeneza chuma.

MAJI

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba jumla ya watu 81,945 kati ya watu 198,269 sawa na asilimia 41.33 wanapata maji safi na salama. Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba hupata huduma ya maji kupitia vyanzo vikuu vitatu, Kama ifuatavyo. i. Maji ya ardhini (visima), ii. Mtiririko wa maji (gravity) iii. Chemichemi za asili

zilizoboreshwa. Katika vyanzo hivyo vya maji kuna miundombinu mbalimbali ya maji kama ifuatavyo;

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba jumla ya watu 81,945 kati ya watu 198,269 sawa na asilimia 41.33 wanapata maji safi na salama. Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba hupata huduma ya maji kupitia vyanzo vikuu vitatu.

Aidha ili kuhakikisha idadi ya watu wanaopata maji safi na salama inaongezeka, Halmashauri imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji vijijini, Ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji 2 vya Chitete na Tindingoma. Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Wilaya ya Momba imetengewa Sh. 1,344,787,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini, ambazo zinatoka kwenye program ya (WSDP-RWSSP).

AFYA

Halmashauri ya Wilaya ya Momba ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 34. Kati ya hivyo vituo vinavyomilikiwa na serikali ni 32 na vinavyomilikiwa na Mashirika ya Dini ni 2. Mchanganuo kwa idadi ya vituo vya kutolea huduma za Afya inajionesha katika jedwali .

Mchanganuo wa vituo vya kutolea huduma za Afya na umiliki wake.

Katika kuhakikisha huduma za Afya zinasogezwa karibu na Wananchi, Halmashauri inaendelea na mkakati wa ujenzi wa zahanati katika Vijiji na ujenzi wa vituo vya Afya kwa kila Kata.

MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINITASAF

Halmashauri ya wilaya ya Momba inatekeleza Mpango wa Kunusuru kaya maskini sana kupitia programu ya TASAF III, Lengo la mradi huu Kuhakikisha kuwa kaya zote katika vijiji 51 kati ya vijiji 72 zilizotambuliwa na kuandikishwa zinahaulishiwa fedha.

Katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa kipindi cha miezi mitatu (Robo ya kwanza) jumla ya kaya 4,132 zenye hali duni zaidi kimaisha kati ya kaya zote 36,912 sawa na asilimia 11.19 zimehaulishiwa fedha kwa lengo la kunusuru kaya maskini ili waweze kujikimu kwenye chakula, malazi, huduma mbalimbali kama vile elimu afya, maji n.k.

Halmashauri ya wilaya ya Momba inatekeleza Mpango wa Kunusuru kaya maskini sana kupitia programu ya TASAF III, Lengo la mradi huu Kuhakikisha kuwa kaya zote katika vijiji 51 kati ya vijiji 72 zilizotambuliwa na kuandikishwa zinahaulishiwa fedha.

Fursa ya ufugaji Wilaya ya Momba.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mathew Chikoti

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Adrian Jungu

Wananchi ka kijiji cha Itumbula kata ya Ivuna wakiwa katika Mandalizi ya ujenzi wa Bwawa la Chumvi

Uvuvi Ziwa Rukwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.