FURSA ZA UWEKEZAJI NA UTALII KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA

Mtanzania - - Fursa, Uwekezaji Na Utalii Nyanda Za Juu Kusini -

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda ilitangazwa rasmi Julai 1 mwaka 2015 kupitia tangazo la Serikali Namba 220, ikiwa na tarafa 02,kata 15,mitaa 43,vijiji 14 na vitongoji 78. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni kati ya Halmashauri 5 zilizomo ndani ya Mkoa wa Katavi. Halmashauri hii iko upande wa magharibi mwa Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ipo katikati ya mkoa wa Katavi katika safu za miinuko ya Katumba miongoni mwa kanda 5 za kilimo za Mkoa huu waKatavi. Manispaa inapatikana kati ya latitude 5o 15’ na 7o 3’ na 1530 kusini mwa ikweta na longitude 30o 31 na 33o00 mashariki mwa Ikweta. Kwa upande wa kaskazini inapakana na Halmashauri ya Wilaya, Mashariki inapakana na Halmashauri ya Nsimbo.

Hali ya hewa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni joto kati kwa sehemu kubwa kwa mwaka. Wastani wa joto kwa mwaka ni nyuzi joto 29 , ambapo hali ya hewa ya baridi inaanza mwezi wa Juni hadi Julai, ikiwa na nyuzi joto 7, Mvua huanza mwezi wa Novemba na huisha mwishoni mwa mwezi wa Aprili. Ikiwa na wastani wa mm 1000 hadi 1200 kwa mwaka zinazoambatana na radi na ngurumo za hapa na pale

Manispaa ya Mpanda ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba of 527 ambapo kati ya eneo hilo kilomita za mraba 30 ni sehemu ya Maji. Kutokana na sensa Agosti 2012 wakazi wa eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni 118,150 Kati yao wanaume ni 58,116 na wanawake ni 60,034. Ongezeko la watu ni 3.6 asilimia kwa mwaka na ina jumla ya kaya 24,275, ikiwa ni wastani wa watu 4.9 kwa kaya. Kwa sasa (2018) Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inakadiriwa kuwa na watu wapatao 146,081 ambapo wanaume ni 71,855 na wanawake ni 74,226 na Kaya 30,014 .

ZAHANATI YA MILALA

Zahanati ya Milala iko katika kata ya Misunkumilo, ikiwa inahudumia vijiji vinne ambavyo ni Kigwa, Shongo, Shuga na Milala na vitongoji kumi ambavyo ni Jeramanga A,B,C,D,E, Katyasho A,B,C, Kigwa na Shongo mabanini. Zahanati hii inahudumia wakazi wapatao 2406 ambapo kati yao wanaume ni 1175 na wanawake ni 1231. ikiwa inatoa huduma za afya ya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua, kama vile huduma za chanjo,elimu ya afya kwa jamii na huduma za upimaji wa VVU kwa hiari. Milala ina watumishi watatu wa kada za tabibu msaidizi, Muuguzi Mkunga na mhudumu wa afya.

Pia Zahanati ya Milala ina miundombinu ya kisasa ikiwamo jengo la kisasa lenye chumba cha mganga, famasia, Stoo, Chumba cha Kujifungualia, chumba cha kupumzika baada ya kujifungua na kusubiria huduma ya kujifungua, eneo la Kliniki ya mama na mtoto, eneo la kusubiri kumwona mganga. miundombinu mingine ni shimo la kutupa kondo la nyuma (placenta pit), kichomataka (incinerator) cha kisasa, mioundombinu mizuri na ya kisasa ya maliwato, Stoo ya Dawa, Samani za ndani na Vifaa vya Kitabibu pamoja na kufunga mfumo wa Umeme wa jua, miundombinu mipya ya huduma iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwezi Aprili 2018 imefanya huduma za Milala kuwa bora.

Hata hivyo Zahanati ya Milala ina nyumba moja ya mtumishi yenye uwezo wa kuchukua familia moja.Aidha Halmashauri ya Manispaa imelenga kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni kuboresha miundombinu ya kutolea huduma, kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba na kuimarisha afya ya kinga, ikianza na kuongeza kasi ya upuliziaji wa dawa za kuangamiza mazalia ya mbu ili kutokomeza maambukizi ya malaria, ugwawaji wa chandarua kwa mama mjawazito na mtoto chini ya miaka mitano na katika shule za msingi na sekondari. Pia elimu imekuwa ikitolewa katika maeneo yote ya utoaji wa huduma ili kuboresha afya za wananchi katika Manispaa ya Mpanda.

Pia Manispaa ya Mpanda imeendelea kupokea watumishi wa kada mbalimbali kwaajili ya kutoa huduma za afya ambapo katika kipindi cha Julai 2017 hadi Julai 2018, Manispaa ya Mpanda imepokea jumla ya watumishi 30 wa kada mbalimbali, ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia uimarishaji wa huduma za afya.

Aidha ujenzi wa Zahanati ya Milala uliibuliwa na Wananchi kwa lengo la kusogeza huduma kwa Wananchi, kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya Mama na Mtoto. Zahanati hii inahudumia Wananchi wapatao 7,174 na inalenga kupunguza vifo vya kinamama Wajawazito na Watoto wenye umri chini miaka mitano ambao awali walitembea zaidi ya Km 8 kufuata huduma za afya katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Mradi huu mpaka umekamilika umegharimu kiasi cha Tshs. 37,000,000.00 kati ya fedha hizo, Tshs 31,000,000.00 ni fedha toka Serikali kuu kupitia Ruzuku ya Maendeleo (LGDG), Tshs 1,000,000.00 toka Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa na Mchango wa Wananchi ni Tshs. 5,000,000.00. Mradi huu ulipokelewa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Kukamilishwa na Halmashauri ya Manispaa mnamo tarehe 12/12/2017.

Katika kutekeleza Mradi huu, kazi zilizofanyika ni kukamilisha ujenzi wa jengo lenye chumba cha Mganga, chumba cha Chanjo, chumba cha kujifungulia, maliwato ya kisasa,

Aidha tunaishukuru Serikali yetu kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambayo imechangia sana kufanikiwa kwa Mradi huu.

MRADI WA WA KISIMA KIREFU CHA MAJI KATIKA KIJIJI CHA MILALA

ujenzi wa kisima Kirefu cha Maji cha pampu ya mkono katika Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo uliibuliwa na Wananchi wa kijiji hiki kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa Maji Safi na Salama na kuwapunguzia akinamama na Watoto adha ya kufuata Maji umbali Mrefu.Halmashauri ina Jumla ya Visima 58, kimojawapo ni hiki kwenye picha hapo juu.

Mradi huu umegharimu kiasi cha Tshs.14,613,000.00 fedha zilizotolewa na Serikali kuu kupitia Mfuko wa Visima Vijijini (RWSSP). Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 25/09/2017 na kukamilika tarehe 25/02/2018, na unahudumia Kaya zipatazo 591.

Katika kutekeleza mradi huu kazi zilizofanyika ni upembuzi yakinifu kubainisha kiasi cha Maji kilichopo, kupeleka sampuli ya Maji ili katika maabara ili kubaini kama Maji yaliyopo yanafaa kwa matumizi ya Binadamu, kuchimba Kisima, kufunga pampu ya kuvuta Maji kwa mkono pamoja na kujenga uzio.

UJENZI WA VYUMBA TATU VYA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI NYERERE

Shule ya Msingi Nyerere ni shule ya Awali na Msingi iliyojengwa Kata ya Kawajense. Shule ipo umbali wa kilomita 06 kutoka Mpanda Mjini. Ni Shule ya kutwa kwa Watoto wa kawaida na wale wenye Mahitaji Maalum. Shule hii ilisajiliwa tarehe 05 Mei,2015 kwa namba EM.16789. Shule ina vyumba vya Madarasa 08 na Jumla ya wanafunzi 3,022 ambao ni kuanzia darasa la awali Mpaka Darasa la saba hivyo kufanya uwiano wa vyumba vya madarasa na Wanafunzi kuwa 1:378. Vyumba tatu vya Madarsa vinavyozinduliwa leo vinaifanya Shule kuwa na vyumba vya Madarasa 11 hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa vyumba vya Madarasa.

Pamoja na ujenzi wa vyumba tatu vya Madarasa mpaka unakamilika umegharimu Tshs 42,244,400.00 kati ya fedha hizo Wananchi wamechangia Tshs 6,192,500.00, Halmashauri Tshs 16,551,900.00 na Serikali kuu kupitia EP4R Tshs 19,500,000.00.

Tunaishukuru Serikali yetu kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda iliyounda timu ambayo ilifanya Mikutano ya kuhamasisha Wananchi kushiriki kwa hali na mali kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa kwa kujenga Maboma.

UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

Shule ya Sekondari Rungwa ni shule inayotoa mafunzo kwa Wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka sita. Ni shule ya kutwa na mchanganyiko kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka nne na bweni kwa wanafunzi wa kiume wa kidato cha tano na sita. Shule ina wanafunzi 1,012 ambapo wanafunzi 926 ni kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne na wanafunzi 86 ni kuanzia kidato cha tano mpaka cha sita.

Ujenzi huu wa Bweni uliibuliwa kwa lengo la kuboresha malazi kwa Wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kuweka mazingira mazuri yanayopelekea wanafunzi kujifunza kwa bidii. Mradi huu umegharimu Jumla ya Tshs 98,311,123 ambapo Mchango wa Halmashauri ya Manispaa kupitia Mapato ya ndani ni Tshs 33,520,000.00, Serikali kuu kupitia ruzuku ya Elimu ni Tshs 59,791,125.00 na Mchango wa Wananchi Tshs 5,000,000.00 Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 24 /06/2017 na kukamilika tarehe 28/04/2018

Katika kutekeleza Mradi huu kazi zilizofanyika ni kujenga jengo ya Bweni, kuweka mifumo ya Maji, umeme na kuweka samani za ndani

UWEZESHAJI WA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI

Pia Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatekeleza sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 na Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000. Sera ya Taifa ya maendeleo ya Vijana inaangalia masuala ya ukosefu wa ajira, umasikini, VVU/ UKIMWI, uharibifu wa Mazingira na matumizi mabaya ya Dawa za Kulevya. Ambapo Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia inaangalia njia za kumwezesha Mwanamke kujiongezea kipato, kujiondolea umaskini na kuwa na maisha bora zaidi. Katika kutekeleza mahitaji ya sera hizo, Halmashauri ya Manispaa imeendelea kuhamasisha uundwaji wa Vikundi ili Vijana na Wanawake waweze kusaidiwa kwa urahisi.

Hata ivyo mpaka kufikia tarehe 02 Mei, 2018, jumla ya vikundi 26 vya Vijana na vikundi 52 vya Wanawake na Kimoja 01 cha walemavu vilikuwa vimeundw vimesajiliwa na kuwezeshwa. Aidha kupitia asilimia 10 ya Mapato ya Ndani, Halmashauri ya Manispaa imeshatoa takribani Tshs 90,000,000.00. kwa Walemavu na kufanya Jumla ya fedha iliyotolewa kwa vikundi kuwa

Sambamba na uwezeshaji wa kifedha, Vikundi hivi pia vinawezeshwa Mafunzo ya Stadi za Ujasiriamali, Elimu ya kuwawezesha Vijana Wanawake na Walemavu kubuni fursa za Ajira na kujipatia kipato. Pia kutengewa maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na huduma. Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda imetenga eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 14,653.509 sawa na Ekari 3.62 katika Kata ya Misunkumilo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali na Viwanda vidogo vidogo. Miundumbinu muhimu kama Maji, umeme, banda la Mlinzi, Choo na Bafu tayari vimekamilika na vinatumika.

UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA MABASI ILEMBO

Mpanda ni Miongoni mwa Halmashauri 18 zinazotekeleza mpango wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Miji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (ULGSP). Katika ufadhili huu Manispaa inatekeleza miradi mikubwa 04 ,Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Mifereji ya maji ya mvua yeneye urefu wa km 4.5 ambao tayari umekamilika , Ujenzi wa Kituo 01 cha mabasi Ilembo, Ujenzi wa barabara kiwango cha lami Km. 7.7 utekelezaji umefikia 80% .

Aidha ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi Ilembo uliibuliwa mwaka 2014 kwa lengo la kuboresha Mapato ya Ndani na huduma za usafiri kwa Wananchi.

Mradi huu umejengwa kupitia mkopo wa fedha za Benki ya Dunia chini ya mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji Miji ULGSP (Urban Local Government Strengthening Programme) mradi huu Umetekelezwa kwa gharama za Tshs, 3,780,614,501.00 kati ya fedha hizo Tshs, 3,451,328,501 ni fedha za ujenzi na Tshs, 329,286,000.00 ni fedha kwa ajili ya malipo ya Mtaalamu Mshauri. Mradi huu umetekelezwa kwa awamu mbili.

Awamu ya kwanza ikiwa ni Tshs. 2,158,984,651.00 na awamu ya pili ni Tshs.1,292,343,850.00, fedha ambazo zinatolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kupitia Mpango wa Uendelezaji wa Miji unaofadhiliwa kwa Mkopo toka Benki ya Dunia. Mradi huu umeanza tarehe 22/05/2015 na umekamilika tarehe 10/11/2017 ,ukisimamiwa na Mtaalamu Mshauri GEOMERTY CONSULTANTS LTD wa Dares salaam na umejengwa na kampuni ya ujenzi ya CHINA HUNAN CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP EAST AFRICA LTD yenye Tawi lake jijini Dar –es Salaam. Hadi sasa Mkandarasi ameishalipwa Tshs, 3,220,995,229.09 sawa na 93 % ya fedha zote na kusalia Tshs, 230,333,271.91 ambazo atalipwa baada ya kukamilisha marekebisho na muda wa matazamio ya mradi.

Aidha katika kutekeleza mradi huu maeneo yafuatayo yamezingatiwa ili kukidhi mahitaji muhimu kama maeneo ya kupumzikia abiria, vyumba 20 vya kukatia tiketi ,vyumba 02 vya mighawa, supermarket 02, chumba cha habari na mwasiliano 01, vyumba vya huduma za biashara mbalimbali 20 na maeneo 02 ya wazi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamiii zinazohusiana na stendi, kituo 01 cha polisi, mitaro ya maji ya mvua, sehemu ya kuegesha mabasi na vyoo vinavyozingatia hali zote. Aidha, Ujenzi huu umekamilika kwa 100% kwa mujibu wa Mkataba na Mkandarasi amekabidhi mradi tarehe 10/11/2017.

Kukamilika kwa mradi huu kutaiwezesha Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kupata Tshs, 20,000,000 kwa Mwezi sawa na Tshs, 240,000,000 kwa mwaka.

UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI IKOLONGO

1. Utekelezaji wa Mradi wa Maji Ikolongo (Mradi wa Vijiji 10) chini ya WSDP I

Halmashauri ya Manispaa Mpanda ilisambazaji maji na usafi wa mazingira vijiji 10 (RWSSP) chini ya mfumo wa WSDP (Water Sector Development Program). Halmashauri ilianza kutekeleza mfumo huu mwaka wa fedha 2008/2009 kwa kuanza kumpata Mtaalamu Mshauri (Consultant),Agosti 2009 mkataba kwa gharama ya USD 173,735.00 sawa Tshs. 232,825,272.20. Na Mtaalamu Mshauri alianza kazi kwa hatua za awali ambapo ilikuwa ni kutambua matatizo ya huduma ya maji hapa mjini kwa maeneo ya pembezoni mwa mji, maeneo yaliyobainishwa ni Kazima, Nsemulwa, Migazini, Misufini, Kasimba, Ilembo, Misunkumilo, Milupwa, Kigamboni na Kivukoni. Pia Mtaalamu Mshauri alifanya usanifu wa mradi wa Ikolongo ambao ndio ulikuwa chaguo la wananchi, utekelezaji wake uligawanyika katika sehemu nne, aliandaa michoro na ramani zote za mradi mtaalamu huyu alilipwa fedha yote Tshs. 232,825,272.20.

Kufikia Juni, 2012 Halmashauri iliingia mkataba na Mtaalamu Mshauri kwa gharama ya Shs. 46,729,796.94 kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi wa mradi wa maji Ikolongo kwa kuanza na ujenzi wa kitega maji Ikolongo na ujenzi wa tanki la maji lita 1,000,000 eneo la Kazima. Kati ya fedha hizo alilipwa Shs. 15,140,577.80 kulingana na kazi alizofanya.

Hata ivyo mwezi Agosti, 2013 Halmashauri iliingia tena mkataba na Mtaalamu Mshauri kwa gharama ya Shs. 205,820,000.00 kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi wa mradi wa maji Ikolongo yaani ulazaji wa mabomba,uliogawanyika katika sehemu tatu za mabomba kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 1. ambao alilipwa Shs. 144,064,925.00 kwa kazi aliyosimamia.

Aidha awamu ya tano ya ujenzi ambayo ilikuwa ni kupanua/ kuongeza mtandao wa mabomba na kukamilisha ujenzi wa tanki, Mapinduzi ilisimamiwa na Halmashauri.

Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji ya mseleleko ya bomba kutoka chanzo cha maji ya chemchemi Ikolongo, uligawanyika katika sehemu kuu tano (5) kama ifuatavyo:

(i) Ujenzi wa kitega maji Ikolongo na tanki la maji lenye ujazo wa lita 1,000,000 (1000m3) eneo la Kazima.

(ii) Ulazaji wa bomba kutoka Ikolongo hadi tanki la Kazima,

(iii) Ulazaji wa bomba kutoka tanki la Kazima hadi Ilembo na vituo vya maji 16,

(iv) Ulazaji wa bomba kutoka tanki la Kazima hadi Milupwa na vituo vya maji 25,

(v) Upanuzi wa mtandao wa mabomba na umaliziaji wa tanki la maji Mapinduzi na ujenzi wa vituo vya maji 8.

Aidha ujenzi ulianza mwaka wa fedha 2012/2013 kwa awamu ya kwanza ya ujenzi ambayo ilikuwa ni ujenzi wa kitega maji Ikolongo na tanki la maji eneo la Kazima. Ulazaji wa mabomba ulianza Julai 2013 na ulikamilika Septemba 2014. Hadi sasa kazi zote zimekamilika.

Kufikia Juni, 2012 Halmashauri iliingia mkataba na Mtaalamu Mshauri kwa gharama ya Shs. 46,729,796.94 kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi wa mradi wa maji Ikolongo kwa kuanza na ujenzi wa kitega maji Ikolongo na ujenzi wa tanki la maji lita 1,000,000 eneo la Kazima. Kati ya fedha hizo alilipwa Shs. 15,140,577.80 kulingana na kazi alizofanya.

Zahanati ya Milala Inaendelea Uk. 15

Meya wa Manispaa Mpanda, William Philip Mbogo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Michael F. Nzyungu

Kituo cha kisasa cha mabasi Ilembo

Utekelezaji wa mradi wa maji ikolongo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.