Bondia Mada Maugo atamba kumaliza pambano mapema

Mtanzania - - Habari Za Michezo / Tangazo - Na GLORY MLAY -DAR ES SALAAM

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, ametamba kumshinda mpinzani wake, Batal Chezhia raia wa Urusi kwa K.O, katika pambano litakalofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bupas Gym uliopo Moscow.

Pambano hilo lisilo la ubingwa litakuwa la raundi 10, katika uzani wa Super middle kg 76.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Maugo alisema anaendelea kujiandaa kuhakikisha anamaliza pambano hilo mapema.

“Mpinzani wangu si bondia wa kunitisha mimi, nishakutana na mabondia wengi nchi tofauti na nimewapiga, naomba tu mashabiki na Watanzania waniaombee ili niweze kurudi na ushindi katika pambano hilo.

“Safari hii nimeongeza umakini zaidi, nimeacha baadhi ya kazi zangu na kufanya mazoezi zaidi, ninajua litakuwa pambano gumu, ila nimeajiandaa kikamilifu kuhakikisha nashinda katika pambano hilo,” alisema Maugo.

– PICHA: MPIGAPICHA WETU

MKATABA: Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Huu Hahn (kulia), na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, wakisaini mkataba wa ushirikiano katika promosheni kunogesha michezo msimu wa Siku Kuu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.