Mkwamba Rangers kutosajili dirisha dogo FDL

Mtanzania - - Habari Za Michezo / Tangazo - Na NYEMO MALECELA - MOROGORO

VINARA wa Ligi Daraja la Pili, Mkamba Rangers, wamesema hawana mpango wa kusajili mchezaji yeyote kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Akizungumza na MTANZANIA jana, kocha mkuu, Nicholaus Makata, alisema kikosi walichonacho hivi sasa kinatosha kuipandisha timu hiyo daraja.

Makata alisema wachezaji walionao wanatosha kuisaidia timu hiyo kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Wachezaji walipumzika siku 10, leo (jana) wameanza mazoezi kwa ajili ya mechi zilizosalia, kwani sasa ligi imesimama kupisha usajili wa dirisha dogo,” alisema Makata.

Makata alisema mbali na kujiandaa na mechi za ligi hiyo, pia wanajipanga kwa mashindano ya Kombe la FA ambalo ratiba yake inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.