Geita, Ambassador Simiyu zasonga mbele Kombe la Shirikisho

Mtanzania - - Habari Za Michezo / Tangazo - Na DAMIAN MASYENENE -MWANZA

TIMU ya Geita Electric ya mkoani Geita imefanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Munanira FC ya Kigoma.

Mchezo huo ulichezwa juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita, ambapo kufuatia ushindi huo Geita Electric watavaana na mabingwa watetezi kutoka Mwanza, Phantom FC.

Kufuatia ushindi huo, Geita Electric ambao ni mabingwa wa Kombe la FA mkoani Geita, watakutana na mabingwa wa Mkoa wa Mwanza msimu uliopita, Phantom FC, Desemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Katika mchezo mwingine, Majimaji FC walitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Ambassador FC ya mkoani Simiyu, baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo huo bila kufungana.

Ushindi huo umeiwezesha Ambassador United kusonga mbele katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ambapo itakutana na mshindi kati ya Twiga FC ya Mwanza na Shinyanga United, ambazo zilitarajiwa kuchezwa leo (jana) jioni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.