Shetta atoa zawadi ya kufunga mwaka

Mtanzania - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongo Fleva, Nurdin maarufu kama Shetta, amesema ngoma yake mpya ya ‘Hatufanani’ ni maalumu kwa ajili ya kufungia mwaka kwa mashabiki zake.

Katika ngoma hiyo ambayo Shetta amewashirikisha Jux pamoja na Mr. Bluu, imeendelea kufanya vema na kushika nafasi ya kwanza katika mtandao wa kijamii wa Youtube.

Akizungumza na MTANZANIA, Shetta alisema baada ya ukimya kidogo ameamua kuuaga mwaka kwa staili hiyo na kuahidi mashabiki zake kusubiri mambo mazuri zaidi kutoka kwake.

“Ukimya wangu ulikuwa kwa ajili ya kujipanga na kutoa kitu kizuri zaidi, huu utakuwa wimbo wa kufunga mwaka lakini pia najiandaa na ‘project’ yangu kwa ajili ya mwaka unaokuja endapo tutavushwa salama,” alisema Shetta.

Aidha, Shetta ameendelea kusisitiza kuwapa kisogo marafiki wasiokuwa na faida katika maisha yake na kuegemea zaidi kwenye familia yake ambayo anaamini ndio kila kitu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.