Babu abaka mtoto wa miaka mitatu

Mtanzania - - Leo Ndani - NA AVELINE KITOMARY

MKAZI wa Mburahati Motomoto, Mohamed Hassan (66), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu (jina linahifadhiwa).

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri, Grace Lwila alidai Oktoba 31 mwaka huu eneo la Mburahti Motomoto Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, mshtakiwa alimbaka mtoto huyo.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na alirudishwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana. Kesi yake itatajwa tena Desemba 19 mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Japhari Ally (30) mkazi wa Manzese Tiptop alipandishwa kizimbani kwa mashitaka ya wizi wa simu.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashitaka, Grace Lwila alidai Oktoba 31 mwaka huu eneo la Manzese Tiptop wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, mshitakiwa aliiba simu ya tecno N8 mali ya Juma Rashidi na kumkata mkono kwa panga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.