Madaktari wa Cuba, Uganda

Mtanzania - - Kanda -

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC) imeajiri madaktari bingwa wabobezi katika maeneo ya upasuaji wa ubongo, moyo, kifua, koo, pua, masikio na njia ya mkojo kukabiliana na upungufu wa wataalamu katika maeneo hayo, anaripoti Clara Matimo.

Mkurugenzi wa BMC, Profesa Abel Makubi, alisema kabla ya kuajiri madaktari hao idara hizo zilikuwa na daktari mmoja au wawili wakati mahitaji ni kuanzia watano hadi kumi kwenye idara moja jambo lililosababisha wazidiwe na idadi kubwa ya wagonjwa.

Alisema upungufu wa madaktari hao wabobezi si kwa Tanzania pekee bali ni changamoto ya mataifa mengi barani Afrika na mabara mengine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.