Dk. Kalemani ahimiza umeme wa Umeta

Mtanzania - - Mkoa - Na FLORENCE SANAWA

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amewataka watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuhamasisha wananchi watumie umeme wa kifaa kitawawezesha kupunguza gharama za kufanya kwenye majengo yao kiitwacho Umeta.

Amesema kwamba, kama watafanikiwa kutumia umeme wa kifaa hicho, watapata umeme unaosambazwa na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea).

Dk. Kalemani alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku mbili aliyoifanya mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa Dk. Kalemani, wateja wengi wana nyumba zenye vyumba vichache, hivyo endapo watatumia kifaa hicho, wanaweza kuharakisha zoezi sambamba na kuepuka vishoka wanaoweza kuwaomba gharama kubwa za kufanya ‘wiring’ kwenye nyumba zao.

“Kifaa hicho kitawezesha wananchi wengi kuanza kutumia umeme kwa kuwa hakihitaji ufanyaji wa wiring pale unapohitaji kukitumia na kinapunguza gharama ambazo awali zilikuwa ni mzigo kwa wananchi.

“Vifaa hivyo vifikishwe kwenye taasisi mbalimbali za Serikali ikiwamo hospitali, shuleni, ofisi za vijiji na kata kwani vitaokoa ghalama za taasisi husika.

“Hamasisheni wananchi watumie hiki kifaa cha umeta ili kurahisha kuwekewa umeme na kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wanaoshindwa kujiunganishia umeme kwa ajili ya gharama hasa ukiwa na chumba kimoja hadi vyumba vine ili kupata nishati ya umeme,” alisema Dk. Kalemani.

Naye Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, alisema kutokana na hali ya mji wa Nanyamba kuwa mpya, kuna haja kwa Serikali kuwawekea umeme wa bei ya Sh 27,000 ili kuhamasisha wananchi wengi kupata huduma hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, alisema uwekaji wa umeme katika vijiji, utaongeza hamasa ya maendeleo kwa wananchi hasa katika Mji wa Nanyamba ambao unakuwa kwa kasi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.