Wananchi waandaa eneo kujenga hospitali

Mtanzania - - Kanda - Na ELIZABETH KILINDI

WANANCHI wa vijijini vitano kata ya mdandu wilayani wanging’ombe mkoani Njombe, wameshiriki kuandaa eneo lenye ukubwa wa ekari 80 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Ihanja, baada ya serikali kupeleka Sh milioni 500 kati ya bilioni moja zinazohitajika.

Akizungumza na wananchi katika eneo hilo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Edes Lukoa alisema awamu ya kwanza tayari imepeleka Sh milioni 500.

‘’Serikali kuu kwa awamu ya kwanza imeleta shilingi milioni 500,naipongeza na kwamba maneno kidogo vitendo zaidi…kwa hiyo hizo zimefika na bajeti ni bilioni moja na milioni 500 na natumai ifikapo tarehe 30 juni mwakani fedha zote zitakua zimefika’’alisema Lukoa.

“Huu mradi ni wa kwenu nyinyi wananchi ni vizuri zaidi mshiriki kila hatua...kuanzia upande wa mafundi hadi kazi nyingine ili tuweze kukalimisha kwa wakati” aliongeza Lukoa.

Kwa upande wa Mbunge wa Wanging’ombe, Gerson Lwenge alisema Serikali itaendelea kuleta fedha kadri ujenzi unapokuwa ukiendelea.

‘’Safari tuliyonayo ni ndefu,fedha hizi hazijaja kama mvua na mkiona vyaelea ujue vimeundwa .... msilete siasa katika masuala ya maendeleo na hivyo tushiriki kikamilifu ili kuweza kukamilisha jambo hili “alisema Lwenge.

Mkazi wa Kijiji cha Ihanja, Alex Mtamba alisema wamejitokeza ili kuandaa eneo ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya ambapo awali walikuwa wakifuta huduma hiyo katika hospital ya kibena mjini Njombe.

‘’ili eneo la ekari 80 tumelitoa sisi wenyewe na kuhakikisha linakua tayari kwa ujenzi tunashukuru serikali kwa kuleta fedha hizi na endapo ujenzi utaanza na kukamilika changamoto za huduma za afya zitaisha… zamani wanawake walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda Njombe mjini ambapo ata wengine walipoteza maisha’’alisema Mtamba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.