Serikali yalia vitendo vya mimba kushamiri

Mtanzania - - Kanda - Na GURIAN ADOLF

SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imelalamikia kuwapo kwa vitendo vya ubakaji wa watoto hali inayosababisha kutopungua mimba za utotoni.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda aliyasema jana, wakati wa kikao kilichokuwatanisha wadau wa mradi wa kupambana na ndoaa na mimba za utotoni kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mradi huo katika mwaka 2018 na kuandaa mpango mkakati wa mwaka ujao.

Alisema kesi nyingi za mimba kwa watoto zinawahusu wanafunzi wanafunzi wa darasa la tatu ambao wana umri wa miaka 13, hali inayo onesha kuwa wamebakwa, hivyo kuna ubakaji mkubwa kwa watoto hao.

Alisema kwa mwaka, kuna ripotiwa wastani wa mimba 100 za wanafunzi kuanzia darasa la tatu pamoja na jitihada zinazofanyika kukabiliana nazo lakini bado imekuwa ni tatizo.

“Najiuliza hata hao watu wanaowapa mimba watoto hao, kweli wanakuwa wamependana na kukubaliana ama wanawabaka, maana haiwezekani mwanaume mzima ukasema umempenda mtoto wa darasa la tatu, hii inaonesha lazima ume mbaka” alisema.

Alisema jitihada zinafanyika kukabiliana na mimba za utotoni kupitia tasisi mbalimbali zisizo za kiserikali ikiwemo Plan Intarnational lakini bado mimba ni nyingi na kuna hitajika nguvu kubwa katika kukabikiana nazo.

Alisema kuna changamoto kubwa kutoka kwa watendaji wa serikali ambao wanapaswa kuunga mkono jitihada za kukabikiana na mimba hizo lakini bahati mbaya wamekuwa kikwazo kutokana na kutofika mahakamani kwaajili ya kutoa ushahidi pindi kesi zinapo endelea.

“Nasema sasa imetosha, iwapo atabainika mtumishi wa umma ambaye anapaswa kufika mahakamani kwaajili ya kutoa ushahidi na asipotoa ushirikiano, mimi kwa kutumia mamlaka niliyopewa na sheria nitaagiza akamatwe na asukumwe ndani kwanza masaa 24 ndipo afunguliwe mashtaka ili sheria ichukue mkondo wake”.

Naye mratibu wa mradi wa kuzuia ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la Plan International, Frank Nestory alisema kuwa hivi sasa ndoa za utotoni zimepungua sana wilaya humo lakini changamoto kubwa ni kwa mimba za utotoni.

Alisema bado jamii wilayani humo haijakubali kikamilifu kubadilika katika suala la kujihusisha na mapenzi na watoto wadogo hali inayosababisha ugumu katika kumaliza suala la mimba za utotoni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.