kukutana na Nkana Rangers

Mbelgiji asema wako tayari kumgonga yeyote atakayejitokeza mbele yao

Mtanzania - - Mbele - Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

WAKATI Simba ikipangwa kukutana na Nkana Rangers ya Zambia katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems, ametamba kuwa tayari ameshaijenga timu yake katika kiwango cha kimataifa, hivyo hana hofu kukutana na timu yoyote kwenye michuano hiyo.

Simba imefanikiwa kuvuka hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, katika mchezo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mavuso, Manzini nchini eSwatini (zamani Swaziland).

Ushindi huo uliifanya Simba kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1, kwani ilipata ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Novemba 28.

Wekundu hao wa Msimbazi watacheza na Nkana Rangers ya Zambia katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini, ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

Nkana ambayo anaichezea Mtanzania, Hassan Kessy, ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha UD Songo ya Msumbiji kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-1, ikianza kushinda

2-1 ugenini, kabla ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani jana.

Simba itaanzia ugenini katika mchezo wa kwanza utakaopigwa mjini Kitwe, kati ya Desemba 14 na 15, kabla ya kurudiana Dar es Salaam wiki moja baadaye.

Mara ya mwisho Simba kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, ilikuwa mwaka 2003 ilipoivua ubingwa, Zamalek ya Misri.

Wekundu hao wa Msimbazi walianza kwa ushindi wa bao 1-0 nyumbani, kabla ya kukubali kipigo kama hicho ugenini, kisha wakaibuka na ushindi kwenye mikwaju ya penalti, ambapo Simba ilitumbukiza tatu, Zamalek ikipata mbili.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems, alisema tayari ameshaijenga timu yake katika kiwango cha kimataifa, hivyo hana hofu yoyote na mpinzani yetote katika michuano hiyo.

“Natambua ubora wao, lakini siwezi kulinganisha na timu yangu, Simba ya sasa ni ya kimataifa, inafanya vizuri, matumaini ya kuwafunga Nkana na kusonga mbele yapo.

“Tungeweza kuwafunga Mbabane mabao mengi, kuna mambo madogo ya kurekebisha kwa washambuliaji wangu, lakini nimepata nguvu kwa kuwa kila mchezaji anapambana kuipa timu mafanikio,” alisema Aussems.

Mbelgiji huyo alifichua siri ya ushindi wa nyumbani na ugenini dhidi ya Mbabane kuwa ni wachezaji wake kuzoea mfumo mpya, licha ya kwamba awali ulikuwa ukiwapa shida.

“Awali mfumo ninaotumia ulikuwa ukiwapa tabu, lakini kwa sasa wanaenda vizuri,” alisema nyota huyo wa zamani wa Standard Liege na Gent za Ubelgiji.

Wakati huo huo, wawakilishi wengine wa Tanzania, JKU ya Zanzibar imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Hilal Ondurman ya Sudan, mchezo wa marudiano

VUTA NIKUVUTE: Winga wa Azam FC, Ramadhan Singano (kushoto), akimpiga chenga beki wa Stand United, Ramadhan Bigirimana, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam juzi. – PICHA: JUMANNE JUMA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.